Habari kwa vina/michano

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
3,489
12,137
Nimekuja huku, na vina bila pozi

Mvumbo ni kapuku, kama ze Bitozi

Twende habari kwa vina, nina maana kuandika kwa kuchana

Iwe habari za kina kinana, ama wana wanaolalama life imebana

Hakuna tabu hata za Magu, mtumbua majipu

Mafisadi tabu weupe kama shabu, siku hizi hawafungui zipu

Karibuni wakongwe mliofuzu, Chlorine gas na Okwi boban sunzu

Mtengwa pia usipite kikauzu, na wengine wote game mnaoimudu
 
Mikono juu...mikono juu..mikono..juu...juu..juu.juu
Piga keleleeee
Unasema mikono juu, badala ya mikono kwenye tunguri

Nakuelewa wewe ni mkuu, wa kupiga buhuri

Na mambo ya kale kuchanja chale, lete kuku na mbuzi weka pale

Na kafara na mchele nazi tele, wanasema nyinyi hamuagizi tembele

Endelezeni tiba, wewe na jichawi

Hapa hakuna msiba, mjumbe hauwawi
 
Nakupata mkuu , vzuri kwa ufasaha

Kijeshi nafunga mguuu, nalianzisha balaaa

Mvumbo tunza bit naanza kuchana kinaaaa

Bro men acha kuramba lips hiz lines zitakupa kinyaaa

Nawapiga xgril wanaojifanya viburi manduri

Mura vaa but vaaa baka tupge section bttle dril

Mvumbo twende pole pole mnyamwezi naanza kupandisha mori
 
Hakuna kudadisi, the gas nazua kesi....

Sizuiliki na polisi, maujanja ka TISS....

Natema flow kali, ka panga lá muuza bucha....

Uzito wa hii mistari, ni Zaid ya Uzito wa busha
Akhsante kwa kuja, mkuu yaani kitambo

Kabla ya pemba na unguja, Jecha kuzua jambo

Na ushindi wa mtutu, waangalizi kuwekwa mahabusu

Hatukuwa watutsi na wahutu, ila amani nusu nusu

Hii ni kabla ya hadithi za majipu, na kabla MCC hawajafunga zipu

Ulipotea kwenye jukwaa letu, sasa ni harakati kama Desmund tutu
 
Tazama hali sio shwari, mapito tunayopita

Mafisadi wanaficha sukari, kumpiga Magu vita

Mkulu nae yupo ngangari, anasema hawawezi kupita

Ila mtaani sio shwari, bei imezidi speed meter

Ukibana huku wao wanatoboa kule

Wenye sauti za kasuku anao kwenye sebule

Tazama wanaochonga, na kujifanya wana dhamira

Maana siku zote kinyonga, hufanana na mazingira
 
Sina uvyama kwenye akili, nawatazama wanaonakili

Hata kama kiongozi tapeli,
ila akisema wanaona kweli

Siasa si hasa wanacheza na hisia

Jifunze kupapasa na pia kufikiria

Mafisadi wapo nchi ya ahadi, wanagawana vyeo

Wamesafishwa maridadi kwa magadi, eti ndio wapo safi leo!!!

Usipende uchama usitende unyama, ili fulani ashinde

Usiende kupigana usijenge uhasama, simama nchi uijenge

Iwapi miadi ya mahakama ya mafisadi, wanatumbua ilimradi mapapa hawawataji

Siasa sio mapambano, kama yanga na simba

Bali ni mtongozano, kubali upewe mimba
 
Ukiwa msela hela nazo ziwe na hela,na ukiwa tozi vipodozi visiote mizizi.tuna moca kama tuko guantanamo,na tuna hekima kama kiongozi flani wa makamo.
 
Pesa ni kama chupi, ipate ikusitiri
Maisha ni mafupi, tenda kwa kufikiri

Lazima ujipange, Ili uepuke majanga

Ni bora uvute bange, kuliko kubwia unga
 
Back
Top Bottom