Habari kuhusu huduma za Luku

msangi360

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
283
308
Huwa nikiwa nyumba ninayoishi Arusha nikinunua umeme wa luku wa sh 10,000/= napewa unit 28. Nikiwa nyumbani nilipozaliwa Moshi nikinunua umeme wa elfu 10, napewa unit 82. Sielewi hii huduma ipoje au kuna nini nifanye kweny luku ya Arusha ili nipate unit nyingi nikinunua umeme wa elfu 10??? Naombeni ushauri
 
Nyumba ya Arusha matumizi yako juu hivyo unazidi unit 75 kwa mwezi hivyo punguza matumizi,kama matumizi yako sawa na ya Moshi Basi kalalamike Tanesco waje waiangalie wakati mwingine mita zinaharibika na kuanza kwenda speed watakubadilishia
 
Mkuu, unachotakiwa kufanya; Nenda Ofisi za Tanesco, watakubalishia hiyo huduma na kukuweka kweny Kundi la Wateja wao wenye matumizi madogo.

Wateja wa Matumizi madogo ni wale ambao hawatumii zaidi ya Unit 70 kwa Mwezi.

Nenda Ofisi zao, ni jambo rahisi sana.
 
Asante sana kwa taarifa
 
Nyumba ya Arusha matumizi yako juu hivyo unazidi unit 75 kwa mwezi hivyo punguza matumizi,kama matumizi yako sawa na ya Moshi Basi kalalamike Tanesco waje waiangalie wakati mwingine mita zinaharibika na kuanza kwenda speed watakubadilishia
Sio lazima nyumba yake ya Arusha ina matumizi makubwa, La hasha...Tanesco wakikuungia umeme kea mara ya kwanza wanakuweka kwenye kundi la matumizi ya kati(ambalo ndo huyo ndugu yupo).

Sasa baada ya hapo wateja wenyewe(Individual wanatakiwa kwenye ofisi zao, na kusema mimi sio wa kundi hilo na wanaweza kuangalia history kama kweli huvuki unit 70 kwa mwezi ndo uunganishwe.
 
Nyumba ya Arusha matumizi yako juu hivyo unazidi unit 75 kwa mwezi hivyo punguza matumizi,kama matumizi yako sawa na ya Moshi Basi kalalamike Tanesco waje waiangalie wakati mwingine mita zinaharibika na kuanza kwenda speed watakubadilishia
Sina matumizi ya zaidi ya unit 75 kwa mwezi, ningekuwa na jiko na pasi Sawa au hita. Ni TV king'amuzi deki, redio, na taa tuu
Ngoja nijaribu kwenda tanesco
 
Ikiwa matumizi yako ni zaidi ya unit 75 kwa mwezi unaingizwa katika group la watumiaji wa kati ambapo elfu 10 unapata unit 28..
Asee yani wananiweka kwenye group la watumiaji wa kati?????!
Maisha yenyew haya
 
Yaelekea ulishatumia kwa mwezi ukazidi unit 75 ndio wakupandishia. Wanasema hata ukinunua umeme kabla ya kupit mwezi na kabla hizo unit 75 hazijaisha unapandishiwa
 
Asee hata kama kuna siku nilinunua umeme kabla ya mwezi hujaisha ntawaambia hiyo siku nilinunua bahati mbaya tu wanisamehe wanirudishe kweny group langu tu hili la kati siliwezi
 
Huwa nikiwa nyumba ninayoishi Arusha nikinunua umeme wa luku wa sh 10,000/= napewa unit 28. Nikiwa nyumbani nilipozaliwa Moshi nikinunua umeme wa elfu 10, napewa unit 82. Sielewi hii huduma ipoje au kuna nini nifanye kweny luku ya Arusha ili nipate unit nyingi nikinunua umeme wa elfu 10??? Naombeni ushauri
Nahisi kutakuwa naluku za chuo Kama vilivyo vifurushi vya chuo, hiyo ndyo picha inayonijia baada ya kusoma post yako
 
Back
Top Bottom