Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,410
- 38,702
Kuna watu wanadai kwa nguvu zote kwamba Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Mchungaji Josephat Gwajima, si Mtumishi wa MUNGU bali ni mpiga dili anayetumia madhabahu ya kanisa lake kufanya siasa. Hoja kubwa ya watu hao ni pale Gwajima anapoonekana kuishambulia Serikali kwa nyakati Tofauti.
Gwajima alianza zamani lakini sauti yake kwa jamii ilianza kusikika wakati wa Mgomo wa Madaktari na wakati ule wakati taifa zima lipo kimya, yeye alimkemea wazi wazi aliyekuwa Rais wa wakati ule pamoja na madaktari waliokuwa kwenye mgomo!
Lakini Gwajima aliamua kwa uwazi kabisa kuonesha kwamba hamuungi Mkono aliyekuwa Mgombea urais kupitia CCM John Pombe Magufuli bali alikuwa anaamini kwamba aliyekuwa anafaa kuwa Rais ni Edward Lowassa kupitia CHADEMA/UKAWA. Na yeye ndiye kwa asilimia kubwa sana alishiriki kusababisha Dr. Willbroad Slaa kuwa huko aliko hivi sasa.
Inawezekana Gwajima anaijua nafasi ya watumishi wa Mungu lipokuja suala la kuwa sauti ya wasiokuwa na sauti(Voice for the Voiceless). Na dini zote mbili kubwa hapa Tanzania, yaani uislamu na ukristo mitume wake walikuwa ni watu wa kupinga uonevu dhidi ya wanyonge wakati wote. Si Mtume Mohamed (S.A.W) wala Masihi Yesu Kristo waliokuwa ni "Vipenzi" vya watawala wa zama zao.
Leo wale wanaosema kwamba Gwajima ni Mwanasiasa na mpiga dili na wala si mtumishi wa Mungu kigezo chao kikubwa eti ni kwa nini "anashambulia" watu badala ya kuwasamehe. Lakini hawa hawasemi ni kwa nini Yesu alipoingia Hekaluni badala ya kuwasamehe wale wachuuzi waliokuwa wanafanya biashara ndani ya hekalu alichukua jukumu la kupindua meza zao na kuwafukuza toka ndani ya hekalu. Yesu alikuwa hana roho ya msamaha?
Hivi Yesu Kristo hakujua kama wale jamaa kufanya kwao biashara mle hekaluni ndiyo walikuwa wanalisha familia zao. Hakujua baadhi yao biashara zao hizo ndizo zinawasaidia Kumpa Kaisari "yaliyo Kaisari" na jee sadaka zao mfumo wa kuzipata haukuwa umevurugwa?
Gwajima si Mwanasaiasa na asisingiziwe kuwa ni mwanasiasa bali ni mtumishi wa MUNGU aliye pia sauti ya wasiokuwa na sauti!!