Kama hayo Magazeti yamempuuza kwa nini na wewe unashindwa kumpuuza?,
Ni wapi umeona Nabii Tito akipewa kipaumbele kwenye vyombo rasmi vya habari zaidi ya mitandaoni?..
.Kwa nini wewe unatamani wawe wanatoa uzito kwa mambo yasiyo na afya kwa jamii kama hayo?.
May Day, kuna hoja ambayo sijui kama wengi wanaielewa! huenda wanaielewa lakini hawataki kukabiliana nayo. Hilo ni tatizo kubwa kwa Watanzania.
Wazungu wanasema 'ukitaka kupata suluhu ya tatizo lazima kwanza ulitambue tatizo''
Hapa kuna sehemu mbili za kuongelea
Mohamed Said anauliza, je ingalitokea maneno hayo kayasema Sheikh, je, magazeti unayosema yangepuuza?
Je, vyombo rasmi unavyosema vingepuuza kama vinavyompuuza Nabii tito?
Je, wangeacha kutoa uzito kwa mambo yasiyo na afya kwa jamii?
Kwahiyo unatakiwa kumjibu Mohamed Said hoja yake kwa mtazamo wa Askofu Gwajima vs Sheikh X
Wakati ukitafakari kumjibu Mohamed, nikukumbushe kuwa kuna kauli kama ''siasa kali, fundamentalist'' , kwamba kauli hizi zinatoka wapi kama tuna uwezo wa kupuuza kila kitu kutoka kwa hawa viongozi wa dini?
Kwa upande wa pili, kuna tatizo kwa Mohamed Said kugoma ku appreciate'' uwepo wa tatizo kwa watu wake
Mathalan, Juzi katiwa ndani Sheikh Ponda . Siku iliyofuata Sheikh Kundecha kakanusha waraka.
Siku iliyofuata shura inakubali waraka huo ni wao.
Katika mazingira haya unawezaje kusema '' waislam wapo kimya' na si kuwa wamepagawa?
Huwezi kuangalia waraka wa Ponda kwa jicho la waraka wa Maaskofu.
Ukifanya hivyo bila kuangalia tatizo la msingi ni kukwepa ukweli.
Kabla ya ulinganifu unatakiwa ujiulize kwanza, je, kuna ulinganifu miongoni mwa watu wako?
Na wala huwezi kuangalia waraka wa Ponda kwa jicho la serikali bila kujiuliza serikali hiyo ipoje madarakani?
Utaratibu wa nchi, serikali inatokana na chama, na chama tawala ni CCM
Nitaendelea nikipata nafasi, nalala niwahi shambani kesho.
Magimbi hapa Magila na Kicheba tumejaaliwa mwaka huu