Gwajima na Manji wananikumbusha yaliyotokea nchini Jamaica

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Kujenga mtandao wa watetezi ni sifa kuu ya watu wanaofanya biashara zilizo kinyume cha sheria, maadili ya kibinadamu au udanganyifu katika nchi masikini kama Tanzania.

Ikumbukwe kuwa kuna umasikini wa aina mbili ambao ni umasikini wa elimu na fedha. Ndani ya umasikini wa elimu kuna umasikini wa mawazo.

Hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa mawazo kwa maana kwamba, hakuna kitu kibaya kama kuikabidhi akili yako kwa mtu mwingine huku pia ukisumbuliwa na njaa na maradhi.

Mjamaica aitwaye Christopher "Dudus" Coke aliweza kutumia umasikini wa wananchi wa Jamaica kujijenga na kupendwa kutokana na kutoa huduma mbali mbali za kijamii kama kutoa chakula, elimu na afya kwa wananchi kutokana na serikali kushindwa kutoa huduma hizo. Pesa za kugharamia huduma hizo alizipata kutokana na biashara ya kuuza madawa ya kulevya.

Wananchi walimpenda sana kiasi kwamba hata serikali ilishindwa kupambana naye kwa sababu hata Waziri Mkuu wa nchi hiyo alitokea jimbo la huyo mfanya biashara wa madawa ya kulevya.

Wananchi wa Jamaica hawakuona athari au tatizo la Christopher "Dudus" Coke la kuuza madawa ya kulevya kwa sababu aliwasaidia kuwapa huduma muhimu za kijamii.

Mfanyabiashara huyo alihakikisha anajenga mtandao ndani ya serikali na chama tawala na pia aliweza kuvizibiti vyombo vya habari.

Serikali ya Marekani ilifikia hatua ya kutoa vitisho kwa viongozi wa Jamaica wamkamate kwa sababu anahitajiwa kwenda kujibu mashitaka nchini Marekani.

Jeshi la Jamaica lilipojaribu kwenda kumkamata lilikuta wananchi kwa maelfu wameizunguka nyumba yake usiku na mchana wakiwa tayari kufa kwa ajili yake. Mapambano yalisababisha zaidi ya wananchi 30 kupoteza maisha achilia mbali majeruhi.

Ukisikiliza Press Conference za Gwajima na Manji utagundua kuwa wanatumia njia hiyo hiyo kama aliyotumia Christopher "Dudus" Coke.

Manji anataka suala lake binafsi liwe ni suala la mashabiki na wapenzi wa Yanga kwa sababu anaisaidia Yanga kifedha. Manji anajaribu kuhakikisha vyombo vya habari vinaandika kile anachokitaka.

Gwajima anataka suala lake binafsi liwe ni suala la waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima kwa sababu anatoa huduma za kiroho na kifedha kwa waumini wake.

Tumeona Manji akiongozana polisi na kundi la mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga.

Tumemuona Gwajima akiongozana polisi na kundi la waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Kwa mpango huu, Manji na Gwajima wanaweza kufanikiwa kwa sababu ya umasikini wa elimu na fedha uliotamalaki nchini.

Je, serikali imejiandaa kwa kiwango kipi katika mapambano yaliyo mbele yake?

A Chinese military general, strategist and philosopher, Sun Tzu once said, If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle.
 
Tatizo bado tuna sheria mbovu za kushugulika na wahujumu uchumi sheria zetu zimelalia kwenye kesi za Uchochezi kwa wanaokosoa serikali"

Mawakili wenyewe kama ndio hao waliokuwa wakiburuzwa mchana na Kibatala basi bora hata tuanze kwanza vetting ya mawakili kabla hatujaingia kwenye hizi kesi ni kujisumbua tu kupoteza rasilimali za nchi "........
 
na ni njia hi2 wanayoitumia ccm na matawi yake kushnda ktk chaguz za hapa tanzania kupitia umaskn wa elimu na fedha! lkn cjui manj na gwajima wame2mia njia hyo tajwa! heb 2one kama kesho hyo gwajima atakuwa amezungukwa na wananch au la ingawa manj sija liona hlo kwa siku ya leo!
 
Ni kweli jamaa wanajidefend kwa kujificha nyuma ya watu, ukisikiliza maelezo ya Mchungaji na mfanyabiashara wote wanatapatapa ,wameshikwa pabaya sana, wanashindwa kujitetea kama hawahusiki kwanini watumie uyanga na kwaya za kanisa ili wawaonee huruma
 
kw kweli mi nashindwa kuelewa kwa nini mambo yao binafisi wayanasibiashe na watu wengine?mi ni shabiki mstaafu lkn siungi mkono kbs hayo mambo yao km wana msala ni bora wawashirikishe gamilia zao lkn sio sisi bana
 
Hili swala la unga selikali inaweza kujikuta inalipa fidia za mabilioni kwakuwazalilisha watu


Mm nimhavidhina wa kupambana na hii vita , ninachotofaufiana na makonda na mdau mleta uzi ni kuweka kando approach sitahiki ya kisheria .aheria ya ushahidi inatamka bayana kuwa ushahidi ufakuwa ushahidi ambao hautacha shaka wala kuweka tashwishi mbele ya mahakama.Kumtuhumu myu bila kuwa na ushahidi ni kumharibu, mbayo kisheria ni kosa la jiana na kisheria kumhatibu mtu.Tupambane na vita hii kwa kutumia rasilimali zote , ili tuwe na ushahisi pasipo shaka na si kuwatuhumu watu bila shaka, mayokeo yake kutakuwa na vita ya kufidia watu bila kuwa na mafanikio na vita halisia
 
Swadakta, hii case study imekaa njema sana.... Una point wewe! Umaskini wa fikra ni umasikini mbaya sana, wa hovyo kabisa.....
Ndivyo nimemaliza hoja yangu kwa kuuliza serikali imejizatiti kwa kiwango kipi katika mapambano?
 
Back
Top Bottom