Gurdiola alidhani EPL ni kama ndondo!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,873
18,433
Gurdiola amelazimika kutoa shikamoo ka EPL! Aliingia kwa mkwala akapiga mechi 5 mfululizo!
Waijuao EPL walijua atachemsha tu! Maana EPL so kama ligi ya ndondo ambayo ligi nzima timu za kueleweka za kuleta upinzani ni tatu tu!
Epl kila timu ni pinzani hata kama inashika mkia!
 
Guardiala tatizo lake ni muoga sana, hasa akiona hapati matokeo. Yeye angebaki bayern tu. Maana Hispania kwenyewe alivyoona Madrid inakuja juu kakimbia.
 
Unayosema kweli kabisa.mi nilivyosikia anaenda man city nilifurahi sana nikajua,ni wakati wake kuonyesha ubora kama coach mwenye uzoefu.Lakin kama unavyosema EPL sio kama spain ambapo christmass mpaka mwaka mpya 'fiesta,' EPL christmass leo kesho uwanjani,mwaka mpya yale yale,tena unapelekwa sehemu kama Bunley au sunderland na kibaridi ndio kimeshika,saa kumi giza ishaingia,lazima body clock ya Guardiola ipoteza mawasiliano kidogo.
Lakin atafanya vizuri,anaitaji mda.
 
Back
Top Bottom