Guninita aonya wanaoitumia CCM vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Guninita aonya wanaoitumia CCM vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 24, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Ijumaa, Agosti 24, 2012 05:47 Na Arodia Peter, Dar es Salaam

  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, amewaonya wanachama wa chama hicho, wanaoigeuza CCM sawa na mali yao.

  Amesema kuwa, tabia ya wanachama hao haiwezi kuvumiliwa, kwa kuwa inakiangamiza chama na pia inakipaka matope chama.

  Guninita aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati akihutubia mkutano wa Baraza Kuu la Vijana, Mkoa wa Dar es Salaam. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za chama hicho, Wilaya ya Kinondoni.

  “Tangu kuanzishwa kwa CCM, chama hakijawahi kushuhudia ubaguzi wowote wa kidini wala ukabila, lakini kadri muda unavyokwenda, kuna dalili ya kuwepo mtandao wa watu wanaotaka kufanya chama kuwa kama mali ya ukoo kwa maslahi yao binafsi.

  “Kuna kamtandao kanaanza kujitokeza, baadhi ya watu wanataka kufanya chama hiki kiwe cha ukoo, hili haliwezi kukubalika, lazima vijana mlikatae kwa nguvu zote.

  “Viongozi wa Serikali ya CCM, akiwamo Rais Kikwete hatuoni familia zao zikijihusisha moja kwa moja kwenye siasa, lakini baadhi ya wanachama miongoni mwetu tunataka kuharibu utaratibu huo, baadhi yetu tunataka chama kiwe mali ya ukoo.

  “Tukifanya hivyo, tunawajengea hofu wasio na ndugu kwenye chama, unakuta viongozi wa ngazi mbalimbali wanatoka familia moja, matatizo hayo yapo, hatuwezi kuyafumbia macho, tunajenga mazingira ya vitisho, alisema Guninita na kushangiliwa.

  Katika hatua nyingine, Guninita ambaye tayari ameshachukua fomu kutetea kiti chake, aliwataka vijana kuwa tayari kujibu hoja za vyama vya upinzani.

  “Nataka kuanzia sasa muanze kujibu hoja za upinzani, msiwaache watambe peke yao, mimi nitajibu zile za Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema), huyo ndiye saizi yangu, nitammudu, lakini si akina Mnyika (John Mnyika, Mbunge wa Ubungo).

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama siku zote Guninita na hao Vijana walishindwa kujibu hoja za CDM leo watawezaje? Lets wait and observe.
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Wale pro SSM wanaonishambuliwa nikisema kuwa SSM ya leo imetuletea ukabila na udini mnaniponda sasa angalieni mwenzeni amesaidia to nail it. Bravo Gugunita!!

  Upande wa pili wa shilingi. Bravo SSM kwa kujimaliza mwenyewe!!! Chasing your own tail!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. p

  pilau JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Guninita anajimaliza mwenyewe hata uenyekiti wa mkoa anaouomba ni tia maji tia maji, amedhihirisha kwamba ni mtu anayekurupuka, alimtukana hadharani Nape wakati anagombea ubunge Ubungo na yeye akawa na mgombea wake Shamsa Mwangunga kwa kauli hizi anazotoa kwamba vijana wa CCM wajibu wapinzani ni katika kujifanyia kampeni kwani siku zote alikuwa wapi?
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hivi huyu Kuninita ndiye nani? Au ndiye aliyekuwa katibu wa CDM aliyeachia ngazi huko morogoro?
   
 6. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Guninita you can't be serious! Mbowe saizi yako? Acha matusi tafadhali.

  Wewe size yako ni mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi au Simiyu na Lindi, Mbowe ni saizi ya Pinda au bosi wako JK maana yeye ni kiongozi wa chama kama JK na ni kiongozi wa serikali ya upinzani bungeni kama Pinda.

  Kukuthibitishia hivyo, kila siku ya maswali kwa PM bungeni basi muulizaji wa kwanza huwa ni mtu waliye size moja ambaye ni Mbowe, unless awe hayupo bungeni siku hiyo.

  Shame on You Guninita!
   
 7. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Ukisikia yalaaa.... ujue limewapata
   
Loading...