lusekelo Andrew
Member
- Dec 10, 2012
- 62
- 19
GUMZO LA DHAMBI YA KUWEKA HADHARANI MSHAHARA WA RAIS
Huku kwenye mitandao ya kijamii, na vyombo vya habari, hasa magazeti, kumekua na mijadala ya kile kinachoonekana dhambi ya kujadili na kuweka kwa hadhara mshahara wa Rais, nimesoma meengi, na kuchangia pia, nami leo naweka mawazo yangu juu ya hili, hapa.
Hivi ni nani mwajiri wa Rais? Ninachokifahamu, kiongozi yeyote aliyewekwa madarakani kihalali na wananchi, na kwa katiba (KISHERIA)akaapa kuwatumikia wananchi wote,tena akijua kua atalipwa fedha kutokana na KODI za hawa aliowaomba kuwatumikia nao wakampima na kukubali awatumikie, basi huyu atakua ameajiriwa na wananchi. Na kwakua mshahara au malipo kwa mwajriwa huwa siri kati yake (mwajriwa) na mwajili wake, kwa tafrisi hii, mshahara wa anaeajiriwa na Hadhara (umma) ni siri kati yake na Hadhara.(Naendelea kutafuta tafrisi ya sheria hii)
Nchi zetu nyingi, za kiafrika, tunapenda kukumbatia usiri katika mambo yanayoathiri au kuathiriwa na umma, na hii imekua moja ya sababu zinazokwamisha uwajibikaji wa hawa viongozi wetu, nani atawajibika katika mazingira ya usiri? Hofu itamkuta wapi, yupo sirini?
Eti leo, mpaka chama cha wafanyakazi serikali kuu sijui, TUGHE nao eti wanalaani kitendo cha mbunge Zitto K kuweka hadharani mshahara wa Rais, kwa kua nao wanaunga mkono usiri-yaani mazingira hasi ya uwajibikaji. Mbona wao wanapopigania ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi mbona wanataja kima cha chini kiwe kiasi gani! Wamesahau! Wamejitokeza kutetea usiri wa mshahara wa Rais, Huu sio unafiki waziwazi?
Historia inatukumbusha, wakati mwalimu Nyerere akiwa Rais, paliwahi kutokea maandamano ya wanachuo UDSM, wakienda Ikulu kwa hoja kadhaa, moja ilikua ni viongozi kua na mishahara mikubwa hivyo kupelekea gap kubwa la kipato kati yao na wananchi, wakati huo mwalimu Nyerere mshahara wake ulikua Tsh 5,000. (haikua siri ndio maana historia ipo), mwalimu Nyerere alipowakaribisha aliwajibu kua anaanza kwa kujipunguzia yeye mshahara wake kwa asilimia 20! (20%), bila shaka hakuona kua hii ni dhambi kwani hawa ndio waajiri wake! Leo hali ni tofauti.
Hivi kujua mshahara wa kiongozi ni haramu kuliko walioficha pesa uswis? Je kunaathiri nini kama tujijua? Nani kaleta hoja ya kutaka Rais au waziri mkuu apunguziwe mshahara baada ya hadhara kujua? Sasa uharamu unatoka wapi? Mimi naamini kua kuna makosa ya kutafrisi hii sheria, au sheria inamapungufu (Naendelea kutafuta msaada wa kisheria ). Ipo haja ya kuachana na usiri, ili kuboresha UWAJIBIKAJI.