Unajua mimi ni mpya katika hii forum ila nilipoona post yako hii kuhusu greenhouse ilinivutia ikabidi tu nitoe hela kidogo niliyokuwa nimeihig=fadhi kwa ajili ya matumizi mengine ili niweze kununua mafunzo yako ya greenhouse. Ila mafunzo yaliyonisaidia kuanza kufanya miradi ni zile dvd zako ulizonitumia kama ofa ambazo ilikuwa ni ya jinsi ya kutengeneza mkaa na nyingine ya kufanya kilimo cha maua hata kama hauna greenhouse. Kusema ukweli sikuwa na ile 600,000 ya kujenga greenhouse hivyo nikaamua nianze na mradi wa mkaa ambao unaweza anza hata ukiwa na sh. 10,000. Nilianza mkaa kutengeneza na kuwauzia washkaji zangu wachoma chips na pesa nilizopata niliweza kuanza kujenga greenhouse yangu. Mpaka sasa nimeshafikia kuanza kupanda mbegu. Mimi nachukua nafasi hii kukushukuru sana kwa zile dvd zako za ofa zimenisaidia sana. Niliamua kuanza mradi wa greenhouse ila nikajishtukia nimeanza na mradi wa mkaa na sasa ndo nimeingia kwenye greenhouse. Naweza kusema nilianza kwa sh. 10,000 kuingia kwenye greenhouse hahaha!