Great thinkers please Help!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Great thinkers please Help!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlachake, Nov 27, 2009.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Jana Kuna dala dala moja ya rafiki wangu wa karibu imekamatwa na maofisa wa TRA ikiwa imebeba abiria aliyekua na box la juice za magendo zenye dhamani ya Tshs 50,000.
  Gari hii inafanya safari zake njia ya Mbeya Tunduma.
  Matokeo yake mwenye gari ameamriwa kulipa fine ya TSHS. 1,200,000
  Hii ni haki?
  mimi shida yangu ni kwa wale walio tunga hii sheria, kwasababu sheria inasema gari yeyote itakayokamatwa na mizigo ya magendo, bila kutofautisha magari ya mizigo na ya Abiria!!
  Je ni jukumu la konda kukagua mabegi ya kila abiria anayeingia kwenye gari?
  Hata kama atafanya ukaguzi. hawa watu wanajanja nyingi!!!!
  kuna case moja, Abiria mmoja aliingia kwenye daladala na sufuria la wali. kumbe chini kaweka vipodozi. jamani nalo hili kosa la mwenye gari?
  case ya pili mama mmoja alikua na mdoli mgongoni kafunga mbeleko halafu ndani kaweka vipodozi, Hili pia kosa la mwenye gari!!! Naomba kuuliza great thinkers, hii ni hakii?
  nawakilisha
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  pole sana ndugu, hii habari ungeibandika pale chini kwenye jukwaa la sheria naimani ungepata ufafanuzi wa KISHERIA zaidi kuliko mawazo ya kawaida!
   
 3. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #3
  Nov 27, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Thanks Mkuu. mod may help on this
   
 4. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #4
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hili siyo kosa la mwenye gari. Kuna watu wengine wanapanda dala dala,halafu wanakwenda kufanya ujambazi,mwenye gari hawezi kulaumiwa. Wengine wanapanda dala dala kwenda kufanya mambo mengine ambayo siyo ya heshima,mambo ambayo hatuwezi kuyataja hapa katika hii Forum ya heshima,hilo siyo kosa la mwenye gari.
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena, na nimekupata!! Lakini Sheria ndivyo inasema. Gari yeyote ikikamatwa imebeba magendo fine kiasi fulani bila kujali kama ni gari ya abiria au la!!!
  mi naona wakati wakwenda kubeba maboksi umefika!!
   
Loading...