Graveyard kinondoni Imejaa.

Graveyard kinondoni Imejaa.

imma_cafelatino

Senior Member
Joined
Dec 5, 2017
Posts
173
Reaction score
178
Wakuu naomba kuwasilisha..

Makaburi ya Kinondoni yamejaa kiasi kwamba hata sehemu ya kuzikia ni shida. Sana Sana unauziwa eneo kinyemela na ndugu yako kuzikwa juu ya kaburi la miaka mingi na ambalo halikujengewa.

Ifike wakati mamlaka husika zizuie watu kuzikwa pale maana ni janga kubwa mnoo.
 
Kwani ardhi ya hapo ina faida gani hasa kwa wazikaji na mzikwaji?
 
Kwani ardhi ya hapo ina faida gani hasa kwa wazikaji na mzikwaji?
Ni ukaribu tu mkuu maana mtu ana mzazi wake au ndugu yake wamekulia na kuzaliwa dar sasa anaona it's better akamuhifadhi ndugu yake karibu ili iwe rahisi kumvisit pindi akijisikia.
 
Waache washupaze Shingo kulifanyia kazi hilo ila wajue hapo ndo mwisho wa Nyodo..,
 
Kujaa waache jiji waseme. Umekagua space ukaona hakuna?
Makaburi hayajai mjini !!
 
Maeneo yote yaliyopimwa yametengewa Eneo la kuzika Sema Demand ya kuzikia kinondoni ni kubwa sana kuliko pengine karibu na maeneo msiba ulipotokea. Suala hapa ni serikali kufanyia kazi hili
 
Makaburi mengi yamejaa kwa sasa. Maana tangu enzi na enzi, watu wanazikwa kila siku, tangu niwe na akili ya kufuatilia misiba mpaka sasa ni mtu mzima, nashangazwa kujua bado mazishi yanafanyika katika maeneo niliyoyajua tangu utoto wangu.
 
Inashangaza mnoo mkuu
 
Cha kushangaza zaidi pale kuna majamaa wanauza maeneo mle ndani eneo la unauziwa 1.5ml kwenye upande aliozikwa kanumba and still kumejaaa na upande huu mwingine wa changanyikeni unapata kaeneo kwa 1ml hv..Naongea haya coz nimeshakumbana nayo.Sasa mbaya zaidi hiyo hela inaingia mifukoni mwa wajanja flani hata hupati tule tu risiti twa kale kamashine kakuleta stress.
 
Back
Top Bottom