Graduates na mlioko vyuoni na shuleni

Graduates na mlioko vyuoni na shuleni

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Posts
11,478
Reaction score
24,250
Mlioko vyuoni na graduates wote mzingatie sana haya mnapoingia kwenye huu ulimwengu sasa..

1. Kiingereza jamani hakiepukiki sasa, jifunze kwa nguvu zote ukiwa shule au mtaani, zaidi ya 60% ya makampuni yanayofanya kazi hapa ni ya kimataifa na jamii tofauti za kimataifa.

2. Jijenge uwe wa kimataifa, usiogope kuwa trainee kwenye international company,hiyo ni nafasi yako ya kuwa wa kimataifa kwa kujifunza standards na tabia za uchapa kazi na uwajibikaji.

3. Facebook, instogram, whatssap, tweeter visiwe ndio sehemu yako ya maisha, tumia mtandao na mitandao kukuza upeo wako na kuijua vizuri taalumu uipendayo.

4. Starehe ukiwa shule sio nafasi yake, ukiwa na hela huku mtaaani starehe utazifanya sana na akina dada au akina kaka wazuri utawapata sana huku, time ya shule fanya shule, huyo uliyekuwa naye anataka android nawe hela huna tutakugongea tu tukuambukize madudu washa.

5. Fanya uchunguzi vizuri wa taaluma unayotaka kuchagua usikalili, soma zile taaluma ambazo zitakazokufanya uwe wa kimataifa.

6. Usije kutegemea serikali kuwa sehemu ya msaada katika future yako, pambana mwenyewe, jitambue mapema ukiwa na umri mdogo nini unachohitaji kwenye future yako.

7. Jenga nidhamu ya maisha.

8. Ukishamaliza shule watoe baba na mama kwenye kichwa chako, mjomba asiwe sehemu ya maisha yako tena.

9. Toa mawazo ya rushwa rushwa kwenye kichwa chako katika kutafuta maisha yako, jifunze kupambana bila msaada wa rushwa, iwe ya ngono au nyingineyo.

10. Egemea kwenye ukweli, uaminifu na uchapa kazi.

Ukizingatia hayo yatakusaidia kwenye maisha yako na taifa lako kwa ujumla.

 
Ushauri mzuri utawasaidia wengi kujielewa.

asante kwa kuliona hilo,,, Tusaidiane kuelimisha ndugu zetu maana tunakaribia kuishi utumwani kwenye ardhi yetu wenyewe..
Vijana wengine elimu ya ufahamu na kujitambua haipo,, mwishowe wanaweza ujinga ujinga tu...
 
Dah, cjui niseme nini kiongozi but umeeleweka

tuisaidie jamii yetu iweze kujitambua, tunapokutana kwenye vijiwe vyetu tuelimishane na kuambiana ukweli mkuu kwani vijana wa kitanzania tumepotoka mkuu na wengi wao hawajitambui kwenye ulimwengu huu wa science na technolojia...
 
Makampuni yanakuja hapa kutafuta faida na si kutusaidia kukua, yatakuhitaji na kukujali ukiwa tu ni productive au unaweza kufundishika,,, vijana wenzangu wa kitanzania tuache kuwa watu wa kusubiri kuhurumiwa.. kijana ukiwa shuleni jijengee uwezo kichwani na si chini ya kiuno, dunia hii ukiwa mzembe utasindikiza wenzio tu. Ni muda sasa wa kutengeneza bongo zetu vijana na kuwa na madini kichwani. Hela zipo hapa tanzania nyingi sana ila zinahitaji uwezo wako tu kichwani na si ugoigoi...
 
Umeongea vyema mkuu, nimekuelewa sana.
 
Mkuu umetema madini
Salute!

thanks mkuu,, ni muhimu kuelimishana maana jamii yetu iko jangani mkuu... tuambiane ukweli kwenye vijiwe vyetu na si kudanganyana na kujazana ujinga tu....
 
thanks mkuu,, ni muhimu kuelimishana maana jamii yetu iko jangani mkuu... tuambiane ukweli kwenye vijiwe vyetu na si kudanganyana na kujazana ujinga tu....

Hii sio kwa walioko mashuleni tu
Hata tuliokuwa mtaani inabidi tubadilike
Again, salute!
 
vijana wengi siku hizivyuoni kiingereza chao ni majanga..yani nkiona tu anavyoandika nawaza akiingia kwenye ofisi itakuwaje?hata barua ya kuomba kazi tu mwajiri akiisoma atashangaa halafu wanalalamika ukosefu wa ajira.ukweli wengi hawapendi kujifunza!
 
Tatizo la aina ya vijana tulionao vichwa vyao wengi wao wanawaza maisha mazuri bila kuwajibika kuyaandaa.
Na wengi wao WANAELEWA KUTOELEWA. Ukisema nao utadhani wanakuelewa, ukimaliza wanayaacha hapo hapo.
How comes kijana hana ratiba, yupo yupo tu.muulize mf.jumatatu ijayo saa mbili ratiba yako vipi? Atakwambia nipo tu kama una sehemu unataka twende basi fresh tutaenda. Yani ratiba zake ni za kukurupushwa tu.Hana ratiba ya muda wa kujisomea for personal development(hata kama ameshamaliza chuo), hana muda kwa ajili ya familia yake, hana muda kwa ajili ya Mungu wake, yeye muda wote ni vijiwe vya kwenye social network, ni admin wa magroup kibao ya kipuuzi.
Inasikitisha sana!
 
Back
Top Bottom