Habari ya leo waungwana. Natumaini wote mu wazima wa afya na mko poa katika kusukuma maendeleo ya Taifa letu pendwa Tanzania.
Bila kuchoshana.
Kama tunavofahamu kumekuwa na ongezeko kubwa sana la graduate au wahitimu wa vyuo katika ngazi mbali mbali kila mwaka, hii imechangiwa na kuongezeka kwa vyuo tofauti na zamani ambapo chuo kikuu ilikuwa Mlimani(UDSM) peke yake.
Ongezeko hili la wahitimu limekuja na tatizo kubwa na sugu duniani kote ambalo ni ajira. Si ajabu kukuta mtu ana miaka mitano, nane au hata kumi toka amalize chuo bado yuko mtaani anatafta ajira na hajafanikiwa bado (inaumiza). Mtu huyu amesoma kwa kodi za watanzania lakini mwisho wa siku hazalishi chochote ila anaendelea kuwa mzigo kwa familia yake na taifa kwa ujumla. Na anaendelea kuwa mazigo kwa sababu elimu aloipata haikumuandaa kupambana na mazingira kwa maana ya kutokutegemea ajira ila ameandaliwa kuwa afisa flani kwenye kampuni kuuuubwa, na anaamini siku moja atakuja kupata huo uafisa.
Wahitimu wenzangu umefika wakati tuamke kwa kujiuliza, je hizo kazi tunazoamini tunazitamani tuzipate je ni kweli tutazipata? Kuna watu wanafanikiwa kuzipata lakini ni 10% out of 100%. 90% tunabaki kulalamika na kusota mtaani maana matarajio makubwa tuliyokuwa nayo hatuyaoni wala hayatakuja daima.
Kwa system iliyopo ajira zimebaki kwa watu wanaosoma nje ya nchi, watoto wa vigogo na walalahoi ambao kwa bahati nzuri wanatoka na distinction GPA pia watu ambao atleast wanamtandao na watu flani ambao wako kwenye system. Jipime je uko kwenye hayo magroup? Mtu ambaye bado yuko chuoni hawezi nielewa sana lakini mtu ambae yuko mtaani ananielewa zaidi ya ninachoongea.
SULUHISHO:
Kuna kampuni ambayo iko katika hatua za mwisho za usajili ambayo itajihusisha moja kwa moja na graduate hasa ambao wako mtaani hawana ajira, wale wanaotarajia kugraduate na wale ambao tayari wako makazini wa fani zote.
Kazi kuu ya kampuni hii ni kuunganisha nguvu kwa pamoja kama wahitimu wa vyuo, kuleta changamoto zilizopo na kuanzisha miradi midogomidogo ya ujasiriamali kwa wahitimu. Kampuni itasimamia uanzishwaji na uendeshwaji wa miradi hiyo ili iweze kuwa sustainable na endelevu. Pia kuhakikisha hakuna graduate anayesota mtaani kwa kulalamika kuwa hana ajira kama atakuwa yuko serious labda aamue kujitenga mwenyewe.
Tumeamua kufungua kampuni kwasababu hata leo ungekuwa na proposal nzuri namna gani ambayo hata ukiwapelekea bank ya dunia wangekusifu na kukupa hela still hawawezi kukupa hela kwa sababu uko peke yako na hauna udhamini ambao utawapa guarantee ya wao kupata hela yao. Kwahiyo utabaki na proposal zako miaka nenda miaka rudi na umasikini ukiendelea kupamba moto.
Hiyo ni kazi moja tu lakini ziko kazi kama tano ambazo kampuni itajihusisha nazo ili kuhakikisha graduate wananufaika.
Tayari kuna wanataaluma(maproffessor), wakuu wa makampuni na taasisi kubwa nchini wameonyesha nia ya kushirikiana na sisi ili kufanikisha adhima hii.
NINI CHA KUFANYA.
Kama unakerwa na hali uliyonayo kama graduate au prospective graduate, tunakukaribisha katika hatua za mwanzo kabia za kuanzisha kampuni hii. Kutakuwa na mkutano mkuu wa kwanza utakaohusisha wadau wote yaani graduate na baadhi ya wadhamni waloonyesha kutuunga mkono, utakaofanyika Dodoma February katikati.
Shiriki kwa kuhudhuria na pia utapata fursa ya kujiunga na kuingizwa kwenye fursa za kwanza kabisa. Katika mkutano huu kampuni itafunguliwa lakini itatajwa miradi ambayo kwa kuanza kampuni itaanza nayo ambayo waendeshaji watakuwa ni graduates.
Kama ungependa kushiriki na kujiunga, pm namba yako katika udhi huu ili uweze kupata updates za yote yanayoendelea.
Katikati ya mwezi huu au mwishoni taarifa zitakuwepo kwenye website ya kampuni ambayo mtajulishwa url(tovuti) yake.
Kwa pamoja tunaweza.
Naomba kiroho safi @Invisible na @mods wautendee haki uzi huu kwa kuupa special attention na bila kuufuta ili kwa pamoja tulijenge taifa letu.
Thanks and welcome.