tumia navigation system mkuuAnayeujua huu utaratibu wa kufunga kitufe kwenye gari ili kukontroo ruti zote anisaidie kunielewesha vizuri.......faida na hasara zake......nataka niitumie sehemu
Mkuu habariAnayeujua huu utaratibu wa kufunga kitufe kwenye gari ili kukontroo ruti zote anisaidie kunielewesha vizuri.......faida na hasara zake......nataka niitumie sehemu
Mkuu shukran sanaMkuu habari
Unafunga katika gari ndogo za kutembea hapa hapa mjini au malori kwa safari ndefu. GPS inasaidia sana. Kwa uzoefu wa kwenye malori una faida kubwa sana hasa kwa malori ya transit kwani inasaidia kutoa
1. Eneo lililopo gari hivyo ni vyepesi kufanya tracking ya eneo halisi dreva alipo
2. Usalama wa mzigo. Kutokana na kufanya tracking mathalani lori limebeba mzigo wa thamani basi utaweza kum control dreva sehemu zipi asimame au apite muda upi
3. Spidi. Vile vile inasaidia kuona dreva anatembea kwa mwendo wa kilomita ngapi kwa saa. Hivyo kama unaona mwendo anaoenda ni tofauti na sera ya mwendo wa kampuni unamtahadharisha dreva apunguze mwendo au aongeze mwendo
4. Kurahisisha katika kuomba mzigo wa kurudi. Hii kwa magari yanayoenda nje ya nchi mfano Zambia. Mzigo wa kurudi unaomba gari ikiwa haijafika mf. Impala, Ndola. Wao wanahitaji kupata daily tracking ripot ambayo itawasaidia kujua lini oda yako iwe tayari sambamba na kufika kwa gari
5. Upande wa mabasi vivo hivyo kumdhibiti dreva na mwendo hatarishi
6. Usalama wa gari lako unakuwa mkubwa. Mathalani gari imeibwa basi ukicheki kwenye automatic tracking report unayoipata kutoka kwenye gari utajua kwa urahisi gari yako ipo wapi hivyo rahisi kuwakamata walioiba gari
Hizi ni baadhi tu wajuzi wengine wanaweza kuongeza
Namna inavyofanya kazi ni baada ya kufungwa vifaa maalumu kwenye gari na kuwekwa line kwa mimi niliwekewa za airtel kwa sababu ya gari kufika hadi Lubumbashi, Congo D. R hivyo frequency zinatupwa katika website na email na simu vile vile ndo upataji wa ripoti
Gharama zake kwa mwaka sisi ilikuwa dola 2000 kwa magari 15