Google kutoa modular smartphone mwaka huu

Joined
Jun 3, 2014
Posts
28
Reaction score
16


Modular smartphone ni nini:

Hizi ni smartphones ambazo zimeundwa kwa dhana ya open hardware (dhana ambayo inashabihiana na open source software kwa upande wa program).

Maana yake ni kuwa mtumiaji anaweza bandika bandua vipande vipande vya components mbalimbali kama spika, skrini, kamera, na kadhalika.

Na hapa hatuzungumzii kutumia bisibisi au soldering gun. Kubadili vipande hivi katika modular smartphone ni rahisi kama tunavyobadili betri, SIM card au memory card katika katika simu nyingi za sasa.

Kitu pekee ambacho kinaweza kubaki bila kubadilika ni fremu pekee ambayo ndio yenye slots za kuchomeka vipande kama unavyotaka.

Kampuni ya Google imekuwa ikiendesha mradi wa kutengeneza modular smartphone ujulikanao kama Project Ara toka mwaka 2013.

Faida za modular smartphones:

Kama ambavyo smartphones za sasa zinamwezesha mtumiaji kuweka app tofauti tofauti kulingana na mahitaji yake, modular smartphones zinatoa uhuru huo kwa upande wa hardware.

Unaweza kuwa na simu ya kivyako vyako kutokana na matumizi yako. Mfano anayependa mobile games akaweka processor yenye uwezo mkubwa,

anayependa sinema akaweka skrini yenye resolution kali zaidi, mpenda music anaweza kuweka external speaker yenye bass kubwa n.k,

hauthibitiwi na hardware kama ilivyo kwenye simu za kawaida kwa sababu kila kipisi kinajitegemea chenyewe hivyo unaweza uka-mix and match kulingana na matumizi yako, kama ambavyo unafanya sasa hivi kwa upande wa apps.

Vipande hivi vitapatikana kupitia soko maalum la Google ambapo watengenezaji na wauzaji watakutana kama ilivyo sasa katika google play store kwa upande wa apps.

Kampuni ya Google imetangaza kuanza kuuza toleo la kwanza la simu hii mwaka huu wakianzia na Puerto rico, marekani.

chanzo: bofyatz.com

 
Daaahhh hizo mambo zimekaa sana.naona ni vema ingehamishiwa kwenye jukwaa.la habari.na hoja mchanganyiko ili wadau wengi waweze pitia hapa
 
Google project Ara imewashinda, kama zilivowashinda Google Glass
 
Google project Ara imewashinda, kama zilivowashinda Google Glass

Google glass haikuwashinda, it just isnt the right time for Augmented reality, wapo enthusiasts ambao they would give $1000 kupata google glass sema bado haijadevelop kivile, 3hrs of battery life ni ndogo mno, bado haina apps za kutosha, AR inahitaji the so called killer app na bado haijapata, consumers wamejaa conspiracy mambo ya piracy kua everytime the camera is watching which is false maana camera ikiwa accessed inawaka taa, n still either people like it or not camera zimejaa kila kona doesn't matter whether mtu ana glass au any other device for that matter if someone wants to find you atakufata tu...

Subiri wakitoa development kit ya Magic Leap hii ambayo google wameifund $500M labda itachange jinsi watu wanavoona AR.
 
nakumbuka chief mkwawa ashaelezea hii kitu siku nyingi kodogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…