Sio tetesi tena, jana Google wametangaza toleo jipya la operating system yao ya android. Toleo hilo ambalo mwanzoni lilijulikana kama android L sasa imethibitishwa kuwa L inasimama badala Lollipop. Pamoja na kutangazwa kwa toleo hili jipya ambalo litaanza kupatikana rasmi kwa watumiaji wa kawaida kuanzia mwishoni wa mwezi wa kumi au mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja, pia Google wametangaza simu na tablet zao mpya ambazo ni Nexus 6 na Nexus 9. Android 5.0 inakuja na msemo wake "Be different. Not the same"
Hebu tupitie machache kuhusu Adnroid L
ANDROID L INATOKA LINI?
Itaanza kupatikana mwezi novemba, pia itakuja na vifaa vipya vya nexus 6 na nexus 9 ambazo unaweza kupre order kuanzia tarehe 17 octoba. Tayari makampuni kama LG, Samsung na HTC wameelezea kuwa tayari kuwapa watumiaji wao toleo jipya la android, ambapo HTC wamethibitisha kuwa wataanza kuitoa android 5.0 baada ya siku 90 tangu ilipotangazwa.
MUONEKANO WA ANDROID 5.0 LOLLIPOP
Hapa Google wamefanya mabadiliko makubwa katika muonekano wa toleo hili jipya la android. Muonekano mpya umetokana na kitu ambacho Google wamekiita Material design. Muonekano mpya ni flat sana kuliko tulivyozoea katika matoleo yaliyopita na kuna matumizi ya vivuli na 3D ili kutofautisha vitu tofauti tofauti.
SYSTEM PERFORMANCE NA MAISHA YA BETRI
Jamaa wa Google wameamua kubali Dalvik runtime, Android's app engine na kutumia mfumo mpya wa ART ambao unasapoti prosesa za 64bit. Hii ina maanisha apps zitarun mara mbili zaidi ya awali. Labda tutegemee kuona mabadiliko katika ufungukaji wa apps kwenye vifaa vya android ambapo uwa inabidi usubili sekunde kadhaa kabla haijafunguka. Gooogle wamedai kuwa wamejitahidi kadri iwezekanavyo kuhakikisha Android Lollipop ina save betri, wameweka machaguo kadhaa ya kupunguza matumizi makubwa ya betri. Pia wamecheza na Graphic engine, hii ni kwa ajili yale HD gaming.
ITAKUBALI KUINGIA KWENYE KIFAA CHANGU CHA ZAMANI?
Anroid 5.0 backward compatibility ina maanisha itaweza kuingia kwenye simu za zamani kabla haijatoka, tayari kampuni ya HTC wamethibitisha kuwa One (M7) na One (M8) zipata, pia Samsung, Sony na LG nao wamesema simu zao zitapata. Pia simu mpya zitakuja na Android 5.0
ISHU YA USALAMA
Google Play itatoa updates kila baada ya wiki sita na itatoa malware definitions mpya, system patches na kitu ambacho watumiaji wengi wa android walikitamani "kill switch" itaweza kuzuia simu isitumike, kufuta taarifa zako pale simu inapopotea au kuibiwa. Hapa sasa ivi wezi wanalo maana simu ikiibiwa itakuwa useless.
nexus ni kwa ajili ya developer watu wamevamia hadi zimeongezwa bei.
motorolla, samsung, htc, lg wote wana play version ambazo ni android ya google.
halafu hio sio android pure bali ni android pure ya google. android pure inaitwa aosp ambayo unaikuta kwenye custom rom kama cyanogen au simu za kichina zisizo na playstore