GOOGLE HATIANI KWA KUZUIA USHINDANI WA KIBIASHARA KUPITIA ANDROID

blogmaster

Senior Member
Aug 15, 2015
167
74
google-673x325.jpg


Muungano wa Ulaya EU umeifungulia rasmi mashtaka ya kujihusisha na vitendo vinavyozuia ushindani wa kibiashara kampuni ya kuhusiana na jinsi kampuni hiyo ya teknolojia inavyotangaza mfumo endeshi wa simu wa android.

Kamishna wa ushindani wa kibiashara katika umoja wa ulaya, Margrethe Vestager ameishutumu Google kwa kuvunja sheria za EU kwa kuwanyima wateja uhuru wa kuchagua na kukandamiza ubunifu.

Google huenda ikapigwa faini kubwa na pia mabadiliko makubwa kufanyiwa mfumo wake wa kibiashara ikiwa itashindwa katika kesi hiyo.

Mfumo wa android kwa sasa unatumika katika asilimia 80 ya simu za kisasa aina ya smartphone zinazouzwa duniani kote.

Tume hiyo ya nchi za Ulaya inaishutumu kampuni ya Google kwa kutumia vibaya ubabe huo.

Bi Vestager amesema kutokana na uchunguzi uliofanywa, Google imekuwa na tabia ya kuwanyima watumiaji wake uhuru wa kuchagua programu endeshi, yaani app, na pia huduma nyingine, na inaathiri ubunifu wa mashirika mengine.

Tume imeguswa kuona kwamba kifaa cha kutafuta cha Google Search Engine ndicho kinachowekwa katika mfumo wa simu zinazotumia android ambazo zinauzwa barani Ulaya.

Imesema, jinsi Google wanavyofanya biashara, na mikataba inayoingia na kampuni zinazotengeza simu kuhakikisha simu nyingi zinauzwa zikiwa na mfumo endeshi wa android, inadhamiria kuzuia washindani wake kuingia sokoni.

Hii ni kesi kubwa ya pili ambayo Tume ya Umoja wa Ulaya imeibua dhidi ya kampuni ya Google.

Kampuni hiyo tayari inakabiliwa na mashtaka ya kupigia debe huduma yake ya manunuzi ya mtandao, kwa kutumia bidhaa za mahasimu wake wa kibiashara.
 
Back
Top Bottom