GOOD: DK Slaa atibua mambo kwa Wassira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

GOOD: DK Slaa atibua mambo kwa Wassira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Feb 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Sunday, 27 February 2011 21:04 0diggsdigg

  [​IMG] Katibu mkuu wa Chadema,Dk Wilbroad Slaa

  Anthony Mayunga, Bunda na Frederick Katulanda, Butiama
  ALIYEKUWA mgombea ubunge wa ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Bunda Elias Maarugu ametimuliwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliohutubiwa na katibu mkuu Dk Wilbroad Slaa baada ya kukataliwa
  na wananchi kwa madai kuwa alihongwa na kumwachia Stephen Wasira.

  Dalili za kumkataa Maarugu zilianza mapema mara baada ya kuitwa asalimie wananchi mjini Bunda, umati mkubwa wa wananchi ulipiga kelele na kudai hawataki kumsikiliza kwa kuwa aliwasaliti na kuuza haki zao.

  Wananchi hao walipiga kelele wakisema hawako tayari kumsikiliza huku wakimtaka atoke jukwaani kwa kuwa hafai, "hatumtaki huyo mtoeni hapo aliuza kura, alihongwa msaliti hafai mtoeni hatutaki kumsikiliza.”

  Kelele hizo zilisikika sauti kwa nguvu za wananchi waliojaza uwanja wa stendi ya zamani.

  Licha ya Maarugu kujikakamua na kusema Peoples, wananchi walipaza sauti na kumtaka atoke haraka sana," hatutaki kumsikiliza huyo mtoeni huyo hafai msaliti alikuwa wapi kwanini amekuja leo siku zote alikuwa
  wapi?”walihoji.

  Kutokana na kelele na wananchi kugoma kumsikiliza Dk Slaa alilazimika kuingilia kati na kusema kuwa, "sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama umma wote huu unakukataa ndugu yangu Maalugu kuna kitu naomba utueleze kwa nini watu hawa wanakukataa.”

  Hata hivyo katibu mkuu huyo kuwataka wananchi wawe na subira wananchi waliendelea kugoma na kusema kuwa hawako tayari kumwona wala kumsikiliza hivyo wakamtaka atoke eneo hilo.

  “Maarugu Chadema inapinga ufisadi ndani na nje ya chama kama unatuhumiwa wewe ni mtu mzima na kuheshimu sana nakuomba uamke taratibu uage uende kwako na sisi tunakuchunguza, natamka kuanzia sasa
  kuwa nakufutia ugombea wa miaka mitano ijayo kwa kuwa hufai maana nakataliwa na wananchi, nitatoa taarifa kwenye kamati tendaji ya chama,”alisema.

  Kutokana na kauli hiyo Maarugu ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Magu na Misenyi alilazimika kushuka taratibu huku akizomewa na maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika hapo,huku Dk Slaa akiwasihi wananchi
  wasimpige,kumtukana kwa kuwa suala lake bado linachunguzwa na wananchi watapewa majibu.

  Aliagiza kamati tendaji ya chama wilaya kuketi haraka kujadili kisha kutoa taarifa kwake ndani ya wiki mbili, na kama wataridhika nayo wataifanyia kazi,vinginevyo watalazimika kuunda kamati maalumya kufuatilia kwa kuwahoji wananchi wa jimbo hilo.

  Mapema Mkurugenzi wa mambo ya Bunge na halmashauri wa chama hicho John Mrema alisema kitendo hicho hakipaswi kuvumiliwa hata kwa viongozi wengine wa chama hicho na kuwa chadema mambo yao yako wazi.

  Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekataa madai ya wakazi wa Tarime kudai kuwa kura zao zilichakachuliwa na CCM kushinda Ubunge katika jimbo hilo.

  Akizungumza jana katika uwanja wa mpira wa barabara ya Nyamwaga, mwenyekiti wa Chadema, alisema hakubaliani na hoja za watu kusingizia chama chake kilishindwa uchaguzi kutokana na kuchakachuliwa kura bali mgawanyiko wa ndani.

  Alisema katika kipindi cha uchaguzi alifika Tarime na kukaa kikao na viongozi wa chama chake Tarime na kubainisha kuwa katika kikao hicho aliwaeleza wazi kama hawajui kushindwa uchaguzi na kama wamesahau kutawaliwa na CCM basi wajue kuwa watajifunza pale ambapo kiti cha ubunge kitakapo ondoka.

  “Niliwaeleza katika kikao cha ndani kama hawajui hathari za ubinafsi basi watajifunza pale watakapopoteza kiti cha Ubunge, niliwaeleza kuwa mtajifunza pale mtakapotawaliwa na CCM. Sasa kuniambia kuwa kura zilichakachuliwa nakataa…sababu naijua,” alieleza Mbowe ambaye alionekana kukasirika.

  Mwenyekiti huyo ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, alisema ingawa alitambua mpasuko huo, yeye akiwa kiongozi wa chama mwenye dhamana ya kupitisha majina ya wagombea, walipoletwa waliogombea waliwapima kwa vigezo na kuamua kulirudisha jina la Waitara Chacha.

  “Leo nalisema hili ili mjue kuwa pale ubinafsi unapotawala katika harakati za ukombozi ni hatari sana…, Mwera alikuwa anataka kuwa mbunge, Waitara, Heche na Matage, wote hawa waliutaka ubunge lakini hawawezi kuwa wote ni lazima ashinde mmoja,” alifafanua.

  Alisema kuwa kila mmoja anayo haki ya kugombea ubunge lakini inapofikia kila mmoja anataka kushinda hapo ndipo inapokuwa ngoma.

  “Nasema tulirudisha jina la Waitara, hatujutii hilo na wala watitajutia. Mwera anaona ahaa…, nadhani hakuridhika, siwezi kujadili mtu hapa na Mwera namheshimu. Basi hapa ndipo ukatokea mgawanyiko na ninyi mkawashabikia mkasahau tatizo siyo mtu bali ni kushinda ubunge,” alisema Mbowe.

  Alisema lakini tokea kumalizika kwa uchaguzi huo watu wakawa wanasema kuwa walisalitiwa na wao kwa wao na wengine kwenda nje ya wilaya kusaidia kampeni jambo ambalo alisema siyo kweli na kusema kwa vile uchaguzi umekwisha sasa ni zamu ya kujipanga na kuangalia walipokosea na kujiandaa kwa uchaguzi.

  “Sitaki kusikia hili la kuchakachuliwa kura Tarime, kama mnadai kuwa mlichakachuliwa kura mlikuwa wapi? Ukerewe ambao walikuwa wakiambiwa mambo kama tarime wameshinda, mabomu yalipigwa lakini wakerewe walikomaa na matokeo yakatangazwa, Mwanza risasi za moto zilipigwa na mabomu usiku kucha siku tatu lakini wakaona looo watangaze sasa Tarime mlikuwa wapi?” alihoji Mbowe.
   
 2. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Imekaa vizuri sana. I am proud to be a CHADEMA member.
   
 3. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  me too!
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  nimefarijika mno pia!
   
 5. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Good ndiyo, hakuna unafiki hapa
   
 6. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Steven Wassira, amemtaka Katibu Mkuu wa Chadema, DK Willibrod Slaa, kutumia elimu yake ya udaktari kuzumgumza mambo ya kitaalamu badala ya kutaka kusikika.

  Wassira alisema kinachofanywa na Dk Slaa ni kutaka kusikika. "Kitendo cha Dk Slaa kupita jimboni kwangu Bunda na kuwaambia wananchi kwamba mimi sifai kwa kuwa nimewasababishia njaa, kinaonyesha anavyoshindwa kutumia taaluma yake kujenga hoja za msingi" alisema Wassira.

  Kwa mujibu wa Wassira, Dk Slaa aliwaeleza wananchi hao kuwa amewaletea njaa licha ya kwamba alikuwa Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji. "Simwelewi DK Slaa, siasa sio kuzumgumza zungumza tu hata kama huna hoja za msingi, kwanza yeye ni Daktari halafu ni mtu mzima, anawaambia wananchi wangu kule Bunda kwamba mimi nimeleta njaa" alisema Wassira na kuhoji:

  "Amefanya utafiti akabaini njaa ya Bunda sababu ni mimi? sasa kuna Jumanne Magembe na Mwanga kuna ukame, je yeye ndio kasababisha?


  Mwananchi Machi 16 2011
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,511
  Likes Received: 2,751
  Trophy Points: 280
  Inaelekea huyu Wassira ni zuzu kwelikweli. Hata anavyongoea inaelekea anafikiri Dr. Slaa ni daktari wa watu!!!
   
 8. f

  furahi JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kama kuna binadamu anayeichukia CHEDEMA kwa moyo wake wote ni huyu baba! Yani anatamani turudi enzi za TANU lol!
   
 9. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inawezekana Wassira hajui what is Politics.
   
 10. d

  ditryman Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanasiasa acheni unafki...
   
 11. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wassira..acha hasira..sababu hasira ni hasara...slaa ni noma...na chadema ni balaaa..watanzania tunaitaka..madaraka tunawapa.:fencing:

  Nawasilisha
   
 12. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wasiira,tuache porojo. Hoja ya msingi hapa ni kilimo cha kisasa kinachopenya season zote na kinachomnufaisha mkulima hata kama mvua haitanyesha. Kilio cha nini wakati tuna mito kibao? Hapo ndipo ilipolala hoja ya dkt slaa. Amkeni jamani kumekucha.
   
 13. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nimefurahishwa sana na hii kitu, kama watu hawakupendi unaachia ngazi mwenyewe, na kama watu wamefahamu kuwa uliuza haki yao huna haki ya kuwa mmoja wao.
   
 14. M

  Makfuhi Senior Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wasira unatakiwa uone aibu. Eneo kubwa la bunda liko mita 5 kutoka usawa wa ziwa victoria lakini wana bunda hawana maji. Kuna sababu ya kuwa na njaa bunda kweli. Shame on you.
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Wasira anakasirika nini si ndio yeye alikuwa anauza sera ya Kilimo Kwanza sasa kilimo kwanza ni kilimo cha kungoja msimu wa mvua kweli naye awe mkweli alipokosea akubali ili afanya bidii wananchi Bunda wafanye kilimo cha umwagiliaji
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Habari murua kabisa. Nadhani Slaa atume watu wa makao makuu ilikuokoa hilo jimbo, maana hilo jimbo si la CCM siku zote ilifikia hatua wakaligawa kwa sababu ya Pressure ya upinzani nilishangaa sana kuona CCM wanalichukua mara mbili wakati hata Wassira aliwai kulipata kwasababu ya Upinzani!
   
 17. N

  Ntandalilo Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimechoka kweli kweli na ujinga wa huyu Wassira hivi anadhani hiki bado ni kizazi cha "zidumu fikra za mwenyekiti na mapinduzi nitakulinda mpk kufa"?!!!!................. haki ya Mungu CCM inaumbukaje mwaka huu? navutiwa na kufurahishwa sana na huu mwamko wa watanzania............ lets go guys ............ lets go......................
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  NIDHAMU YA WOGA...
  Waswahili hutafsiri nidhamu ya woga kama - UNAFIKI. Hili ndio tatizo kubwa la viongozi wetu pamoja na kundi kubwa la wananchi wa Tanzania..
  Habari hii nitakuja itafutia mida niandike kitu safi kuhusiana na na somo hilo hapo juu...Nidhami ya Woga.
   
 19. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Alikuwa Upinzani kwanini Alirudi Chama Tawala? Umaarufu wake uliisha???
   
 20. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  peoples..................power
   
Loading...