Hii imenikumbusha kuwa tuko safarini, siku wala saa tusioijua Mungu atatuhitaji.............tujiandae. Moyo wangu unasikitika pamoja na familia yake ya nyumbani na Jf family pia. Ni ngumu kukubali hali halisi kibinadamu lakini ndio hakuna rufaa. Moyo wangu pia uko kwa mtoto wake mzuri aliyetuachia, namuombea faraja pekee ya Mungu imfariji, Mungu ampe walezi wazuri watakao mjali, kumthamini na kumpenda.