Godoro La Mtumba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
Mjomba aliitikia shikamoo yangu huku akinitumbulia macho. Nilihisi kuna zaidi ya tatizo, haikuwa kawaida yake kuniangalia kwa macho ya vile.

Nilijiuliza kama nina kosa nitakimbilia wapi maana ndani ya nyumba tulikuwa tukiishi wawili tu. Mimi na mjomba Msafiri. Yeye alitengana na mke wake mama Muna miaka minne iliyopita.

Wakati wanatengana mimi nilikuwa bado nyumbani, Ngamiani Tanga nasoma Shule ya Msingi Usagara. Baada ya kumaliza

darasa la saba, nilikosa nafasi ya kuendelea na masomo ndiyo akanichukua mjomba, kaka yake mama yangu.

Mjomba Msafiri alinichukua mwaka mmoja mbele baada tu ya kutengana na mama Muna. Mama yangu yaani dada yake

mjomba ndiye aliyemuomba kunichukua kuja kusoma hapa Dar.

Alinitafutia sekondari binafsi ipo maeneo ya Ubungo Kibangu. Sasa hivi nipo kidato cha tatu.

Maisha yetu nyumbani na mjomba yalikuwa mazuri sana, nyumba nzuri, ina geti, mjomba ana gari, msichana wa kazi na mlinzi. Mjomba anafanya kazi kampuni ya wazungu.


"Shani," mjomba aliniita kwa sauti iliyojaa utulivu wa hali ya juu baada ya kumaliza kuniangalia kwa kunitumbulia macho.

"Unajua wajibu wako uliokuleta Dar es Salaam?"
"Najua mjomba," nilimjibu huku nikichekacheka.

"Ni nini?" aliniuliza akiwa amekunja uso kuashiria kwamba hanitanii.

"Kusoma."
"Unasoma?"
"Nasoma mjomba."


Haya Tena Baada ya kumaliza Sherehe za sikukuu ya Eid El Fitri ninawaleteeni Kitu kipya hicho hadithi ya kusisimuwa mukiipenda mubonyeze neno hili
(Like) hapo chini nitajuwa munaipenda na nitaiendeleza musipo bonyeza neno (Like) sitoweza kuendelea kazi kwenu wapenzi wangu.........
 
Tunaisubiria kwa hamu, simulizi hilo jipya...

Btw mkuu MziziMkavu wewe na Zahra White iko dugu moja ama? mbona nyie mutu mbili naandika swahili inafanana fanana!
 
Last edited by a moderator:
Tunaisubiria kwa hamu, simulizi hilo jipya...

Btw mkuu MziziMkavu wewe na Zahra White iko dugu moja ama? mbona nyie mutu mbili naandika swahili inafanana fanana!
Mkuu watu8 bana wewe iko na matatizo sana. Mimi bana sina udugu na mkuu.@Zahra White niupate wapi huo udugu mkuu watu8 wewe ni mtu wa wapi hapo Danganyika?
 
Last edited by a moderator:
Kweli mukuu, vile wewe na Zahara munaandikaga ni kama dugu moya..
Mkuu Dr.zero Una muunga mkono Mkuu watu8 maneno yake? Kiswahili changu ninacho kiandika wewe unafikiri ni cha wapi? Ki-Rwanda au Ki-Kongo au kiswahili cha kihindi au Kiswahili cha Kizungu ninaomba unijibu hapo? Angalia maandishi yako uliyoandika yenye rangi nyekundu hicho ndio kiswahili safi Mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu watu8 bana wewe iko na matatizo sana. Mimi bana sina udugu na mkuu.@Zahra White niupate wapi huo udugu mkuu watu8 wewe ni mtu wa wapi hapo Danganyika?

Hahaha...nimependa namna unavyoumba sarufi hususani panapohusisha konsonati 'm' ikiambatana na irabu 'u'
 
Last edited by a moderator:
Asante sana bana mukubwa mkulu watu8 hongera sana nisamehe bana kama nimekosea kuandika kiswahili lugha ya taifa.

Hapana mkuu wala usijali...niliileta hii porojo ili kuchagiza tu hii mada tupate kutanua zetu mbavu kwa kicheko cha bashasha...
 
Godoro La Mtumba - 2-


Mjomba aliitikia shikamoo yangu huku akinitumbulia macho. Nilihisi kuna zaidi ya tatizo, haikuwa kawaida yake kuniangalia kwa macho ya vile.

Nilijiuliza kama nina kosa nitakimbilia wapi maana ndani ya nyumba tulikuwa tukiishi wawili tu. Mimi na mjomba Msafiri. Yeye alitengana na mke wake mama Muna miaka minne iliyopita.

Wakati wanatengana mimi nilikuwa bado nyumbani, Ngamiani Tanga nasoma Shule ya Msingi Usagara. Baada ya kumaliza darasa la saba, nilikosa nafasi ya kuendelea na masomo ndiyo akanichukua mjomba, kaka yake mama yangu.
Mjomba Msafiri alinichukua mwaka mmoja mbele baada tu ya kutengana na mama Muna. Mama yangu yaani dada yake mjomba ndiye aliyemuomba anichukue kuja kusoma hapa Dar.
Alinitafutia sekondari binafsi ipo maeneo ya Ubungo Kibangu. Sasa hivi nipo kidato cha tatu.
Maisha yetu nyumbani na mjomba yalikuwa mazuri sana, nyumba nzuri, ina geti, mjomba ana gari, msichana wa kazi na mlinzi. Mjomba anafanya kazi kampuni ya Wazungu.
“Shani,” mjomba aliniita kwa sauti iliyojaa utulivu wa hali ya juu baada ya kumaliza kuniangalia kwa kunitumbulia macho.
“Abee mjomba.”
“Unajua wajibu wako uliokuleta Dar es Salaam?”
“Najua mjomba,” nilimjibu huku nikichekacheka.
“Ni nini?” aliniuliza akiwa amekunja uso kuashiria kwamba hanitanii.
“Kusoma.”
“Unasoma?”
“Nasoma mjomba.”
“Zaidi ya kusoma shuleni mnafundishwa nini kingine?”
“Mh!” niliguna kwanza.
Nilijua swali la mjomba lina maana, halikutokea vivi hivi tu.
“Mjomba kwa nini umeniuliza hivyo?” nilimuuliza na mimi. Si unawajua Watanzania, swali linajibiwa kwa swali.
“Wewe una uwezo wa kuniuliza badala ya kujinibu?” mjomba alikuja juu.
Nilimwangalia mjomba kwa macho ya tofauti na siku nyingine, alitisha sana siku hiyo.
“Tunafundishwa masomo tu,” nilimjibu.
“Mnafundishwa masomo tu?”
“Ndiyo mjomba.”
“Sasa mbona wewe unajua na mambo mengine?” mjomba aliniambia huku bado macho ameyakaza kwangu.
“Yapi mengine ninayoyajua mjomba?” nilimuuliza huku nikijiangalia nilivyo.
“Yapi? Nani unamuuliza swali hilo, we mwehu nini?”
Nilijua mjomba amekereka sana na jambo, hajawahi kunitukana hata siku moja, mara zote mjomba amekuwa akinionesha upendo wa hali ya juu, nadhani hapendi nijione naishi kwa upweke kwa sababu siko na wazazi wangu.
“Samahani mjomba kama nitakuwa nimekukosea, lakini naomba nijulishe kosa langu. Mimi wakati natoka nyumbani Tanga kuja kwako, mama aliniambia wewe ni sawa na baba yangu.”
Niliposema maneno hayo ndipo nilipomwona mjomba akirudi kwenye sura ya kawaida…
“Unajua Zuwena mimi naishi na wewe kama mwanangu, unapokwenda kinyume lazima niwe mkali, au nakosea?”
“Hukosei mjomba.”
“Oke, nafurahi kama umelitambua hilo. Eee, unatakiwa uwe unajua nini cha kufanya ili watu walisikutafsiri vibaya, sawa?”
“Sawa mjomba, nashukuru kwa ushauri.”
Mjomba aliondoka eneo hilo na kuniacha mimi tu. Nilikwenda chumbani kwangu nikajitupa mtoto wa kike, puu.
Mawazo yakanijaa kichwani. Kwamba, ndiyo nimemshukuru mjomba, lakini je nimemshukuru kwa lipi?
Kosa langu ni lipi? Nilipitia mambo mengi niliyoyafanya siku hiyo au jana yake ambayo yanaweza kusababisha aniseme, lakini nilikosa majibu.
“Unajua Zuwena mimi naishi na wewe kama mwanangu, unapokwenda kinyume lazima niwe mkali, au nakosea?”
Haya maneno yaliniumiza sana na yalikuwa yakijirudia akilini mwangu mpaka basi.
“Hukosei mjomba.”
“Oke, nafurahi kama umelitambua hilo. Eee, unatakiwa uwe unajua nini cha kufanya ili watu walisikutafsiri vibaya, sawa?”
“Sawa mjomba, nashukuru kwa ushauri.”
Moyo uliniuma sana, nilitamani kwenda kumuuliza mjomba kwa mapana, tatizo ni lipi, maana naweza kuwa naishi lakini kumbe ishu ni kubwa.
Ilifika mahali nikaanza kuhisi kwamba huenda mjomba kaambiwa maneno fulani na mtu ambayo hayana ukweli ndani yake.
Siku hiyo ikakatika, kesho yake nakumbuka ilikuwa Jumamosi, mara nyingi Jumamosi mjomba huwa anarudi nyumbani na demu wake, anaitwa Zuhura Chachandu.
Huyu mwanamke simpendi kama nini! Ana tabia ya kujishebedua sana. Akija mara zote lazima nikose raha.
Atakwenda chooni, bafuni, jikoni na uani, akirudi lazima atasema mi mchafu, simpendi!
Mjomba alitoka akisema atachelewa kurudi….
“Mjomba leo utarudi na Zuhura Chachandu?” nilijikuta nimemuuliza mjomba hivyo swali ambalo alionekana kulishangaa.
“We Zuwena tangu lini ukaniuliza swali kama hilo? Halafu yule kwako si Zuhura Chachandu, ni anti, sawa?”
“Sawa mjomba.”
Mjomba alipoondoka nilibaki najiuliza mwenyewe, ni kwa nini nilimuuliza mjomba vile? Ni kweli hata siku moja sijawahi kumuuliza swali kama lile.


Itaendelea baadae......... Mkuu Mtambuzi like mbona ni moja tu?
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu mpaka uendeleze sehemu ya 3 ndio ntakupa like. Nasubiria hapa.
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu hebu endelea kutukonga mioyo bhana!

Hadithi nzuri na nataka nitabiri hapo mbele itakuwaje lakini ngoja niache kwanza.

Like
 
Last edited by a moderator:
Kule kwa shigongo nilimiss sehemu ya 3, mzizi ilete hapa fasta
 
Mkuu MziziMkavu, huyo Mdada kwenye BOLD RED si anaishi maeneo ya TANDALE KWA MKUNDUGE.......?
Si yule ambaye aliwahi kufumaniwa na SKUANZA MIYE BINTI MAMBALIGWA MSHAMU wa KISIJU, akang'atwa sikio la kushoto mpaka leo anaitwa Zuhura Chachandu Kisikio...

Au siye huyo......?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…