Godfrey Zambi amesaini?

Deofm

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
383
68
Huyu jamaa hajasaini azimio la kuiwajibisha serikali, lakini angalia anavyopiga kilele kudanganya wapiga kura wake.

Alisema hoja ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu ilianzishwa na wabunge wa CCM katika kikao chao, hivyo hawatarudi nyuma mpaka wahakikishe mawaziri wote wanaotuhumiwa wameondolewa madarakani.

"Unajua hoja ya kutokuwa na imani imeanzishwa na wabunge wa CCM kwenye kikao chetu cha ndani, wapinzani waliichukua baada ya kupata siri yetu, lakini hilo halijalishi kwani wote tumeungana kwa pamoja kupiga vita ufisadi," alisema Zambi.

Alisema sasa katika suala la kupiga vita ufisadi ni la wabunge wote wa CCM, na aliwataka wananchi kuona mabadiliko makubwa kwani ile tabia ya kuona kila mwaka serikali inatumia vibaya fedha na wao kuunga mkono, umeshakwisha
.
 
Kama hajasaini adhabu yake ni kuzomewa na wapiga kura wake hadi atakapojiuzulu ubunge mwenyewe.
 
Weston zambi ni mpenda 2mbo kama fisi anaenyemelea mkono upi udondoke atambae nayo.Huyu mpiga soga na analinda maslahi yake kipara huyu
 
Zambi anautamani sana uwaziri cku nyingi ndio maana anauma na kupuliza anataka kuwaridhisha wapiga kura na kuibembeleza serikali ili apewe angalau unaibu waziri!! hopeless chap!!
 
Back
Top Bottom