Godbless Lema na mwisho wa fungate (Honeymoon)!

MTK

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
8,927
6,850
Awali ya mengi; nichukue fursa hii adhimu kukupongeza kwa dhati kwa kufanikiwa kutetea kiti chako cha Ubunge wa jimbo la Arusha mjini; tunafahamu umeruka na kuvuka vikwazo na changamoto nyingi sana na za kutisha (2010-2015); kuelekea ushindi wako huo uliotukuka; hongera sana.

Wakazi wa Arusha na kwingineko tunafahamu na kuelewa kwamba vikwazo, vitisho na changamoto lukuki ulizozipitia kwa namna moja au nyingine huenda vilikunyima nafasi na uwezo wa kuwatumikia wananchi kwa maana ya kubuni na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kadri ya matarajio ya wana-Arusha na penginepo hata wewe mwenyewe ambavyo ungependelea kufanya.

Nichukue fursa hii kukuhakikishia kwamba Usife moyo; sisi wapiga kura wako tilikuelewa vizuri sana kwa sababu tumekuwa mashuhuda wa majanga mbalimbali yaliyokuwa yakikusibu na ndio maana tumekurudisha kwa kura nyingi kama ishara ya kutambua juhudi zako. Waingereza wana kamsemo kaendako hivi; nanukuu: "to every cloud there is a silver linning"; nyuma ya mateso, jasho na maumivu yako umeasisi jimbo lenye watu wenye kujitambua, jasiri, imara na wanaozijua vema haki zao na wenye utayari wa kuzitetea kwa hali na mali na ikibidi kwa damu zao! Asante sana Godbless Jonathan Lema.

Sasa awamu ya kupigania uhuru na ukombozi wa fikra kwa wananchi wa Arusha mjini IMEKWISHA! The honeymoon is over Mr Lema! sasa tuko huru, tunajitambua na tuko tayari kwa awamu ya pili (2015-2020); kwa ajili ya kujiletea maendeleo kwa kutekeleza mabadiliko katika mifumo ya utendaji na utoaji huduma, tunataka kuona mabadiliko katika huduma za jamii, miundombinu ya maji, umeme na barabara, huduma bora za afya, shule bora zenye madawati, usafi wa jiji, masoko, mazingira na huduma za kiungwana katika taasisi za umma nk.

Kwa kifupi sasa unaingia katika awamu ya kufanya kazi kwa "KASI ZAIDI, WELEDI ZAIDI na UMAKINI ZAIDI" ili kuyafanya matunda ya kazi yako yaonekane DHAHIRI bin SHAYIRI kwa wakazi wa jimbo Arusha wote bila kujali vyama wala itikadi kwa sababu maendeleo hayana itikadi! Katika awamu hii mpya (2015-2020) Mheshimiwa Lema hauna kisingizio chochote kile! Wewe ni mbunge, umepata meya na naibu wake na madiwani lukuki, kwa pamoja mnadhibiti halmashauri ya jiji na kamati zake zote, Mungu akupe nini?

Nyenzo unazo kilichobaki ni kuonyesha uwezo wako na kuthibitisha kwamba harakati zako dhidi ya udhalimu wa ccm zilikuwa na nia njema na sababu thabiti.

Nachelea kusema kwamba kazi yako adhimu ya kujenga hamasa ya kujitambua miongoni mwa wana arusha uliyoifanya kwa weledi na umahiri mkubwa sana inaweza kugeuka bakora ya kukuchapia wewe mwenyewe endapo utashindwa kuelekeza nguvu zako, raslimali watu na fedha kutuletea mabadiliko ya kweli katika maisha ya wakazi wa jiji hili!!

Kuna haja ya wewe mwenyewe kuongoza dhana ya mabadiliko ya kweli kwa kuzingatia kwamba siku hazigandi; funga fungua 2020 hiyoo hapo! Ukituangusha hakuna jinsi utakavyoweza kutushawishi tukuchague tena 2020, hakuna!!! tutakuchapa tu; Utafyatuliwa uondoke period; UTAPIGWA TU!
Mwisho ninakutakia afya njema na maono mapya ya mikakati endelevu kwa ajili ya mabadiliko ya kweli wakati huu unapoelekea kuanza awamu mpya ya uwakilishi wa jimbo la Arusha.

Wathibitishie wanaarusha na umma wa watanzania kwamba Unaweza. Kama jina lako; may GOD the almighty BLESS you manyfold in this new phase of your political career.

GJL; its your time to write a lasting Legacy to the people and city of Arusha; Go for it Lema; the sky is the limit Lema! Peeeeeoples!

MTK@0622/0673-211 770
 
Asante wana Arusha kwa kuwakomesha majambazi. Waliwapiga risasi za moto na kuua ndugu zenu. Wamemua kipenzi chenu Alphonce Mawazo, lakini ninyi mkasubiri muda muafaka mkawasurubu
 
Tunaimani amesikia na atafanya kazi zaidi, kwani pamoja na kupitia vipindi vigumu ameweza kusimamia mapato yakaongezeka na matumizi kwa kiasi fulani alisimamia kikwazo ilikua uongozi wa ccm, lakini tumeona kazi kubwa tu ambayo ameifanya huku kwetu barabara ilikua hakuna tulikua na makorongo ya mito, mvua ikinyesha hata kwa mguu kufika nyumbani ilikua shida, lakini sasa kuna barabara ya changarawe tunaimani itawekwa lami huvi karibuni. miaka zaidi ya hamsini ilikua ni ndoto kuona barabara na km 8 kutoka ktk ya jiji, na lazima tuelewe kwamba yeye ni mbunge na madiwani, ila raisi na mawaziri bado ni ccm, lazima tujue mipaka ili tusije laumu hajafanya kumbe pesa za bajeti hazijaletwa na serekali itoe pesa za kutosha na kwa wakati tuwahukumu kama watashidwa kubuni na kusimamia miradi na matumizi ya budget.
 
Ebana eeh mi ata Lema akiiba au kuaribu poa ni bora na yy kuliko izi stress za maccm na huu umeme wao,2020 kura yangu ni kwa Mungu mbariki Lema atake asitake
 
Mkuu umeongea point sana. Lema huu muda ndo wa kuweka jina na kuionyesha Tanzania kuwa faida ya kuichagua chadema ni ipi. Hii inahusu pia halmashauri zote 34 zinazoongozwa na chadema. Make a difference!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom