Godbless Lema kuiteka Dodoma leo

Godbless Lema kuiteka Dodoma leo

Polisi mkoani dodoma wamezuia mapokezi na mktano wa mbunge wa Arusha mjini mh. Godbless Lema, sasa kuingia kimya kimya..

.....

kwani wewe ulikuwa unategemea nini zaidi ya kuzuia mapokezi na mkutano chezea polisi wa CCM wewe.
 
Lema hawezi kuiteka Dodoma, sema Lema kufanya mkutano Dodoma.

......

Tatizo lako unachangia thread ukiwa na stress za mtwara.Halafu sio kila post lazima uchangie. Nyingine unaweza zikaushia pia.
 
Kazi ipo,ccm wapo tayari kupingana na nguvu ya umma kwa kutumia vyombo vya dola. Kila lililo la heri wana dom!
 
Kwanini, mbona Mandela tulimpokea kwa maandamano.

Na Clinton kule Arusha mpaka barabara za lami zilipigwa deki lkn maandamano ya wazalendo yanasababisha usumbufu kwa watumiaji wengine. Wanajisumbua tu ni vigumu sana kumzuia mtu kukipenda akipendacho.
 
Viva Lema viva vava, Aluta Continunue, mapambano bado yanaendelea.
 
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbles Lema wa Chadema, anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa mjini Dodoma baada ya kupokewa kwa maandamano yanayotarajia kuanzia Ihumwa kilomita 14 kutoka Dodoma Mjini.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma mjini, Jella Mambo, ilieleza kuwa msafara wa Lema utaanzia katika Kijiji cha Ihumwa ikiwa ni safari yake kuja bungeni.

Lema ataingia Dodoma na kutinga bungeni baada ya kushindwa kushiriki mikutano mitatu ya Bunge baada ya kuvuliwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka jana.

Hata hivyo, Desemba 21 mwaka jana, mbunge huyo machachari alirudishiwa ubunge wake baada ya jopo la majaji kuridhika na sababu za rufaa yake na kumpa ushindi kuwa ni mbunge halali za Jimbo la Arusha Mjini.

Mambo alisema jana kuwa mapokezi ya Lema yatakuwa ni makubwa kuliko mapokezi yoyote ambayo yamewahi kufanyika katika Mji wa Dodoma na kuwa yataongozwa na msafara wa mapikipiki, magari pamoja na msururu mrefu wa watu.

Katibu huyo alisema kuwa mara baada ya kuingia mjini Dodoma, msafara wa Lema utakwenda moja kwa moja Ofisi za Chadema mkoa ambako mbunge huyo pamoja na msafara wake watakwenda kusaini kitabu cha wageni.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mara baada ya kusaini kitabu msafara huo utakwenda katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Central ambako hakutakuwa na jambo lolote litakalofanyika zaidi ya utambulisho na kisha mbunge huyo kupewa nafasi ya kuhutubia mkutano wa hadhara utakaoanza saa 10 jioni.

Kwa muda wa wiki sasa viongozi wa Chadema wa ngazi ya mkoa na wilaya wamekuwa wakihaha kwa kufanya maandalizi ya mkutano huo.

Mji wa Dodoma una hekaheka kubwa na umepambwa kwa bendera mbalimbali za chama cha CHADEMA ishara inayoonyesha mapokezi hayo kuwa ya kutisha na yakihistoria katika siasa za mkoa huu.

Source:Mwananchi Jumanne

Namkubali sana kijana Lema hasa kwa kuwa na ujasiri wa hali ya juu aiyeogopa mtu yeyote!!!
 
Watu wengine bwana sijui ni wivu au nini ukweli ndio huo nyota inangaa kubali yaishe
 
Lema hawezi kuiteka Dodoma, sema Lema kufanya mkutano Dodoma.
​mtasema saana lakini uongo na ukweli havikai sehemu moja poleni na mambo yenu ya utapeli wa mtwara
 
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbles Lema wa Chadema, anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa mjini Dodoma baada ya kupokewa kwa maandamano yanayotarajia kuanzia Ihumwa kilomita 14 kutoka Dodoma Mjini.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma mjini, Jella Mambo, ilieleza kuwa msafara wa Lema utaanzia katika Kijiji cha Ihumwa ikiwa ni safari yake kuja bungeni.

Lema ataingia Dodoma na kutinga bungeni baada ya kushindwa kushiriki mikutano mitatu ya Bunge baada ya kuvuliwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka jana.

Hata hivyo, Desemba 21 mwaka jana, mbunge huyo machachari alirudishiwa ubunge wake baada ya jopo la majaji kuridhika na sababu za rufaa yake na kumpa ushindi kuwa ni mbunge halali za Jimbo la Arusha Mjini.

Mambo alisema jana kuwa mapokezi ya Lema yatakuwa ni makubwa kuliko mapokezi yoyote ambayo yamewahi kufanyika katika Mji wa Dodoma na kuwa yataongozwa na msafara wa mapikipiki, magari pamoja na msururu mrefu wa watu.

Katibu huyo alisema kuwa mara baada ya kuingia mjini Dodoma, msafara wa Lema utakwenda moja kwa moja Ofisi za Chadema mkoa ambako mbunge huyo pamoja na msafara wake watakwenda kusaini kitabu cha wageni.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mara baada ya kusaini kitabu msafara huo utakwenda katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Central ambako hakutakuwa na jambo lolote litakalofanyika zaidi ya utambulisho na kisha mbunge huyo kupewa nafasi ya kuhutubia mkutano wa hadhara utakaoanza saa 10 jioni.

Kwa muda wa wiki sasa viongozi wa Chadema wa ngazi ya mkoa na wilaya wamekuwa wakihaha kwa kufanya maandalizi ya mkutano huo.

Mji wa Dodoma una hekaheka kubwa na umepambwa kwa bendera mbalimbali za chama cha CHADEMA ishara inayoonyesha mapokezi hayo kuwa ya kutisha na yakihistoria katika siasa za mkoa huu.

Source:Mwananchi Jumanne
kitu cha kuangalia kwa makini ni vitu vyenye ncha kali kutoka kwa magamba
 
Back
Top Bottom