Godbless Lema kuiteka Dodoma leo

Godbless Lema kuiteka Dodoma leo

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbles Lema wa Chadema, anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa mjini Dodoma baada ya kupokewa kwa maandamano yanayotarajia kuanzia Ihumwa kilomita 14 kutoka Dodoma Mjini.


Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma mjini, Jella Mambo, ilieleza kuwa msafara wa Lema utaanzia katika Kijiji cha Ihumwa ikiwa ni safari yake kuja bungeni.


Lema ataingia Dodoma na kutinga bungeni baada ya kushindwa kushiriki mikutano mitatu ya Bunge baada ya kuvuliwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka jana.


Hata hivyo, Desemba 21 mwaka jana, mbunge huyo machachari alirudishiwa ubunge wake baada ya jopo la majaji kuridhika na sababu za rufaa yake na kumpa ushindi kuwa ni mbunge halali za Jimbo la Arusha Mjini.


Mambo alisema jana kuwa mapokezi ya Lema yatakuwa ni makubwa kuliko mapokezi yoyote ambayo yamewahi kufanyika katika Mji wa Dodoma na kuwa yataongozwa na msafara wa mapikipiki, magari pamoja na msururu mrefu wa watu.


Katibu huyo alisema kuwa mara baada ya kuingia mjini Dodoma, msafara wa Lema utakwenda moja kwa moja Ofisi za Chadema mkoa ambako mbunge huyo pamoja na msafara wake watakwenda kusaini kitabu cha wageni.


Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mara baada ya kusaini kitabu msafara huo utakwenda katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Central ambako hakutakuwa na jambo lolote litakalofanyika zaidi ya utambulisho na kisha mbunge huyo kupewa nafasi ya kuhutubia mkutano wa hadhara utakaoanza saa 10 jioni.


Kwa muda wa wiki sasa viongozi wa Chadema wa ngazi ya mkoa na wilaya wamekuwa wakihaha kwa kufanya maandalizi ya mkutano huo.

Mji wa Dodoma una hekaheka kubwa na umepambwa kwa bendera mbalimbali za chama cha CHADEMA ishara inayoonyesha mapokezi hayo kuwa ya kutisha na yakihistoria katika siasa za mkoa huu.

Source:Mwananchi Jumanne
 
wish you all the best Lema. najua Lukuvi huko aliko ana mbwela mbwela tu akijua jembe limerudi mjengoni
 
Namkubali sana Lema, ingawa simuamini kwa aslimia 100
 
Mtujuze yatakayojiri,naipenda CDM mimi,je wewe?
 
Lema hawezi kuiteka Dodoma, sema Lema kufanya mkutano Dodoma.
 
Nasi wana Moro 2meandaa msafara mkubwa wakwenda naye kamanda we2 wa kwe
 
Polisi mkoani dodoma wamezuia mapokezi na mktano wa mbunge wa Arusha mjini mh. Godbless Lema, sasa kuingia kimya kimya..
 
Hofu ni jambo baya sana kwa binadamu yeyote ambaye hajiamini,waliozuia mapokezi wanaogopa kuona mwitikio wa wananchi utakavyokuwa wakati wa mapokezi na kuonesha Lema anakubalika hata na wana Dodoma
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Dr. Rehema Nchimbi alishapiga MARUFUKU mikutano ya hadhara na maandamano MKONI MWAKE wakati wa vipindi vya BUNGE (Wakati BUNGE likiwa kwenye session).

Je hiyo ban imekuwa lifted lini? Just for curiosity.
 
Back
Top Bottom