Kwako Mheshimiwa Lema
Tukio la tarehe 31/October, 2011 la wewe Kukataa Dhamana hivyo kulazimika kwenda rumande katika Gereza la Kisongo kwa siku 14 limezungmzwa na Watu wengi sana na mpaka sasa limekuwa ni Gumzo sehemu mbali mbali za nchi yetu. Wapo waliokupongeza kwa uamuzi wako na wako waliokupuuza kwa Uamuzi wako kila mmoja akitoa sababu zake.
Tukio ulilolifanya tarehe 31/October, 2011 limenifanya nikumbuke tukio lililotokea tarehe 16/October, 1953 katika Viunga vya Mji wa Havana Cuba kipindi cha Utawala Dhalimu wa Dikteta Fulgencio Batista. Ilikuwa ni Siku Fidel Castro alihukumiwa kwenda jela kwa Miaka kumi na tano kwa kosa la Uhaini. Katika kuhitimisha Speech yake ndefu aliyoitoa Mbele ya mahakimu waliokuwa wanamhukumu Fidle Castro alisema
I know that imprisonment will be harder for me than it has ever been for anyone, filled with cowardly threats and hideous cruelty. But I do not fear prison, as I do not fear the fury of the miserable tyrant who took the lives of 70 of my comrades. Condemn me. It does not matter. History will absolve me.
Maneno hayo ya Fidel Castro yamebeba ujumbe sawa kabisa na Maneno haya katika speech yako
wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu.
Ni maneno ambayo kama CCM na Serikali yake wangejua kwamba utakataa dhamana na kutoa huo Ujumbe basi usingepata
Bahati ya kukamatwa. Nasema Bahati maana Tukio la kukamatwa kwako limekuwa Bahati Mbaya kwa Watawala na hakika Mtawala yeyote angejua nini kilikuwa kichwani mwako Angekupuuza wala asihangaika na wewe.
Umekataa KUONEWA, umekataa DHULUMA, Umekataa MANYANYASO, Umetoa Ujumbe kwa wale wote wanatishwa na Magereza kwamba Hakuna Mahabusu inayoweza kuhifadhi UMMA kwa Pamoja, kwamba DHULUMA ikizidi sana BINADAMU anaweza akamfata hata Polisi mwenye Silaha. Nakumbuka wakati Red Indians wanadai uhuru kutoka kwa Mwingereza, walilala kwenye Reli Kupinga MANYANYASO na kudai UHURU na Haki na hata Dereva wa Treni wa Mwingereza alipopita Juu ya MIILI yao hakuna aliyeondoka reline hata Pale Derava alipoona kwamba Asingeweza kuwasaga Wote na Kusalimu Amri.
Wengi wanaokuponda eti wanadai wewe ni mkorofi, Umefanya Maandamano bila Kibali, Ni wapuuzi tu maana wanafikiri Watanzania na wana Arusha hawakuona wale viwavi jeshi wa CCM a.k.a UVCCM walipofanya Mikutano na Maandamano Haramu chini ya OCD Fedhuli Zuberi, wanaokuponda wengi wetu ni Wasomi ambao wanafurahia hii AMANI feki ilihali Mama zetu
wanajifungua kwa shida, Watoto zetu wanasoma katika mazingira Magumu, na Vijana wengi wanazidi kukosa Ajira na Maisha ya Mtanzania yanazidi kupanda.
Nakupa Moyo Mh. Lema kwa Sababu UNAUNGWA MKONO na kundi ambalo halina Cha Kupoteza, Unaungwa Mkono na Makundi ya Watanzania waliopigika Kimaisha, Kundi ambalo Wapondaji wako akina Ngongo wanaliita ni Kundi la
Jobless, kundi la wavuta Bangi , kwamba wote wanakuunga Mkono ETI WANAITWA Wavuta Bangi, lakini nikutie Moyo tu kwamba Hata Yesu alipokuja Duniani alisema
Sikuja duniani kwa ajili ya Watakatifu bali wenye Dhambi ili wapate kuokoka, Kwa hiyo unapoona kwamba Unaungwa mkono na Wavuta bangi wengi, Jobless wengi usihudhunike maana hiyo inaashiria kwamba saa ya Ukombozi I Karibu Maana hata waliomngoa Gadaffi au Mubarak walikuwa ni Jobless na Wavuta bange kama wapinzani wako wanavyowaita.
Moto Uliouwasha ni Mkubwa na Kwa Kweli serikali ijiandae kujenga Mahabusu Nyingi maana watu sasa Hawataogopa Mahabusu, hawataogopa Risasi.
Mungu Akuabriki sana
Wako Katika Mapambano, Albedo
Please Mod: naomba kwa heshima na Taadhima msiiunganishe hii thread maana nimeiadress kwa Mheshimiwa Lema. asante