Countrywide
JF-Expert Member
- Mar 2, 2015
- 21,193
- 33,580
Habari wanajf, leo kuna jambo ambalo nimeona lina ukakasi sana kuhusu Lema.
Lema ameondoka nchini kwa sababu vitisho anavyopewa kwa mujibu wake mwenyewe.
Inaweza kuwa kweli au la, lakini ambacho nimeshindwa kukielewa ni kuwa lema ameondoka na familia yake (mke na watoto wake tu) na hatujui lini atarudi maana wanaomtisha wanaweza kuendelea kumtisha kwa muda mrefu.
Hapa nimebaki na maswali mengi sana, pale nyumbani kwa lema kuna ndugu pia, kuna mtoto wa mawazo( yeye mwenyewe ndio alisema anamlea mtoto huyu nyumbabi kwake).
Leo imetokea hatari/vitisho kwake, kakimbia na mke na watoto wake tu, je hawa wengine nao wakimbilie wapi?
Na mara ulipokuwa kenya ukasema Tanzania hakuna uhuru wala haki na kuna ukiukwaji wa haki za binadamu.
Tuseme sawa, ila sisi ndugu zako wa damu kwa kabisa(mashangazi, wajomba, baba wadogo, wakubwa na watoto wa dada, kaka) wao wana haki ya kukandamizwa ila watoto wako hawana hiyo haki?
Kama kukimbia manyanyaso hapa Tanzania na ukiukwaji wa haki za binadamu basi ungeondoka na sisi pia ndugu zako wa karibu, au sisi sio binadamu? Sisi tuna haki ya kukandamizwa?
Wale uliowaacha pale nyumbani kwako arusha sio binadamu wale? Au wale hawakandamizwi?
Pia nimeshangaa sana, siku ya october 30, ulipost jambo la kishujaa sana kwa kusema "nipo tayari kwa lolote, sitaogopa vitisho vyovyote" , " tunatakiwa kumuogopa Mungu tu na sio binadamu"
Iweje leo usema unaogopa vitisho na waksti ulishasema hivyo sio lolote kwako, hakuna wa kukutisha ukaogopa? Leo hii unaogopa binadamu kuliko Mungu?
Au haya umesahau kama uliyasema?
Yote kwa yote, nina amini kuna kitu umejifunza na tumeshakusamehe sisi ndugu zako.