GNS3 -Part II (Loopback adapter) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

GNS3 -Part II (Loopback adapter)

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kilongwe, Jan 30, 2011.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Video ya makala hii inapatikana HAPA

  Siku za karibuni,tuliongelea umuhimu na ukuaji wa vifaa au programu zinazoweza kufanya kazi za vifaa kamili(simulators),mfano mmojawapo ni kwa wale watu wa mambo ya mawasiliano ya computer(Networking),kuna moja ya programu ambayo hupenda kutumia inayoitwa GNS3.

  Kwa kutumia programu hizo,unaweza ifanya kompyuta yako kufanya kazi sawa na kifaa halisia,sasa je unajua ni ninsi gani unavyoweza kutengeneza anuani ya loopback na kukuwezesha kuiunganisha netiweki yako na ulimwengu? Leo hii nitakuelezea kwa hatua chache tu unaweza kufanikisha hili.

  1.Nenda kwenye search na andika 'cmd',kutatokea kijiboksi cheusi,andika hdwwiz.exe ,vilevile kwa wale wanaotumia Windows 7 za halali unaweza kwenda search na kuandika hdwwiz.exe moja kwa moja.

  [​IMG]


  2.Itafungua kijiboksi kipya cha kuongeza hardware kama inavyooonekana kwenye picha ,bofya next

  [​IMG]


  3.Katika machaguo mawili,chagua hilo lililoandikwa install manually


  [​IMG]


  4.Kukishafunguka kibokso kipya,kokota chini kabisa na uchague network adapters


  [​IMG]


  5.Upande wa kushoto wa manufacture chagua Microsoft,na upande wa kulia kokota mpaka upate Microsoft Loopback Adapter,na uichague


  [​IMG]


  6.Bofya next ili kuanza kusimika,itachukua kamuda kutegemeana na nguvu ya kompyuta yako.  [​IMG]

  7.Itatumia muda kukamilisha msimiko,baada ya hapo bofya finish ili kumaliza,unaweza hitajika kuianzisha upya kopyuta ili kuifanya ifanye kazi

  [​IMG]


  Matatizo: Kwa wale ambao wapo kwenye maofisi au mashule,mara nyingi sana ili kuzuia upoteaji wa bandwidth ama sababu za kiusalama huwa tunafanya kitu kinachoitwa IP-MAC binding,hii inamaana, kifaa kinachoruhusu wewe kuingia online(authenticator) kinatengeneza chati ambayo ina IP na MAC husika .

  Sasa,ili kuhakikisha mtu aliyejiunga ni yuleyule,huwa tunaweka muda fulani(MAX age ) ambapo kila baada ya huo muda mtumiaji anatakuwa kujisajili tena,hii hufanyika chini kwa chini. Hivyo kitu kitakachotokea ni kuwa loopback nayo itaanza kutuma paketi na kumfanya msajili aone unaongopa na kukupiga chini. Hivyo wasiliana na Administrator wako kwa msaada.

  Muhimu:Angalia ujumbe ambao unaweza kupambana nayo,hii imenitokea kwenye kompyuta ambayo nimeinganisha na campus network.
  [​IMG]
  Kama unaona huitaji,basi hakuna haja ya kuiondoal,unaweza kuizima tu kwa kwenda system Management->Hardware halafu utaangalia kwenye network card halafu bonyeza mbonyezo wa kulio na kuchagua disable,ukichagua Uninstall ina maana umeiondoa.

  Ni hayo tu kwa leo wakubwa nikitegemea mutakuwa mumepata angalau kidogo.
   
Loading...