Global Imperialism on the rise!

Kama hukuwa unajua basi ujue kuwa Marekani hayupo kwa sasa kwenye mashambulizi ya Libya, alishajitoa upo hapo?

Mkuu tazama mlolongo wa matukio yote.
Huu ukoloni mamboleo unarudi kwa kasi sana, na kuwepo au kutokuwepo na Marekani katika ACTUAL attacks hakuondoi dhamira ya nchi za magharibi kutaka kuitawala Libya na mafuta yake.
Naungana na only83 katika kuchambua suala zima.
Precedence iliyowekwa na nchi za magharibi ni mbaya sana kwa nchi za dunia ya 3.
 


mwenzake Mubarak hakuwa na ndege za kivita? Mbona hakuwaita raia wake mende? Mbona hakuamuru ndege za kijeshi zitumike Takhrir Square? Qaddafi na Mabeberu wote lao moja...hawana mapenzi mema na watu wa Libya. Qaddafi haamini kitu kinachoitwa demokrasia, ndiyo maana mpaka kesho anakataa kuitwa rais (anataka aitwe kiongozi).

mtu asiyeamini democrasia hawezi kuruhusu nguvu ya umma katika utawala wake. acha wamtwange.
 
Kama hukuwa unajua basi ujue kuwa Marekani hayupo kwa sasa kwenye mashambulizi ya Libya, alishajitoa upo hapo?
Mkuu.
US hajajitoa.

Yet Gates, asked whether the military operation might be over by year's end, said, "I don't think anybody knows the answer to that."
At least one of the five Navy ships and submarines that have launched dozens of Tomahawk cruise missiles at Libyan targets from positions in the Mediterranean Sea has left the area, three defense officials said. They spoke on condition of anonymity in order to discuss sensitive military movements.
That still leaves what officials believe is sufficient naval firepower off Libya's coast, and it coincides with NATO's decision Sunday to take over command and control of the entire Libya operation. Aided by international air power, Libyan rebels were reported to have made important gains by capturing two oil complexes along the coast.

Clinton, Gates: Libya Operation Could Last Months
 

kwanza si kweli kwamba Mubarak hakuua Waandamanaji, zaidi ya Wamisri 300 walikufa katika maandamano yale.
pili waandamanaji wa amani hawawi na silaha za kulipua vifaru, silaha za kulipua ndege, n.k

Tatu azimio la kulinda wananchi wa libya inaonekana Nchi za magharibi wanalitumia kusapoti waasi wakati hawatakiwi "kutake sides". hii inaonyesha malengo yao yanakwenda beyond kulinda civilians, bali kutoa air cover kwa waasi ili wamng'oe Gadafi. na hii kusema kweli ni precedence mbaya sana, next time watatumia excuse hiyo hiyo ya kulinda Civilians ili kutoa kipondo kwa nchi hasimu zao kama Iran na nyinginezo.

Kwa mtu yeyote mpenda Uhuru wa Kujitawala hana budi kulaani kitendo cha nchi hizi kuconspire kuipiga Libya. na ili kujua unafiki wa nchi hizi, hawataachia waasi kuichukua Tripoli kwa nguvu , watalazimisha mazungumzo baina yao na Gadafi, ili Gadafi asije akacollapse kienyeji kienyeji na hatimaye kusababisha Chaos ya Civil war ambayo lawama na Gharama zitawarudia wao. hii air operation wanayoifanya ni kujaribu kuwa na "upper hand" kwa wote, waasi na Gadafi, kwa waasi watahakikishiwa mikataba minono ya mafuta, na kwa gadafi atawahakikishia anaondoka salama, ili kuwapoza wafuasi wake wasiendeleze armed struggle, iwapo Gadafi atakamatwa na majeshi ya waasi au hata kuuawa. wewe Subiri uone.
 
umejaribu kuchambua ila unatia shaka pale unaposhindwa kuona tatizo la Gadaff kwa jinsi ambavyo alideal na hili tatizo la waandamaji,mara al qaeda then waasi.Yes US wanaonea lakini kwa nini unambeb Gadaff kama malaika wakati ana move kibao za kigaidi????????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…