Anaandika Mwamba wa Kaskazini
Leo nimefurahishwa na busara nyingine ya Mzee Lowassa na kuusikitikia tena na ujinga wa Mbowe.
Watu hawa wawili leo wamefanya mambo mawili tofauti na kwa nyakati tofauti yanayotuachia wosia muhimu katika siasa za nchi.
Wakati Lowassa kaendeleza siasa za maendeleo kwa kuhudhuria ufunguzi wa maktaba kubwa UDSM, mahali aliposoma, Mbowe yuko gerezani ambako ni matokeo ya ujanja ujanja wake wa kukiuka sheria na ndiko mahali anakoisoma namba.
Wawili hawa leo wanatupa fundisho kubwa nalo ni moja tu; hoja sio kubadili gia bali unabadilishia wapi?gerezani au mlimani!
Mwaka 2015 kila mtu anajua kuwa Mbowe alipiga hela ndefu akamsaliti mwanamageuzi wa kweli Dr. Slaa.
Wakati wengi mwaka huo wakidhani Mbowe alikuwa mwanamageuzi wa kweli leo wamejionea kuwa ni tapeli na msanii wa kisiasa wa karne ya 21.Ndio maana hakuelewana na wanasiasa wote wanaohoji akina Chacha Wangwe, Zitto Kabwe n.k na sasa wabunge wengi wamemkimbia na baadhi ya waliomo ndani wamemchunia.
Anaongoza chama kisicho na ajenda yoyote kwa sasa kisiasa zaidi ya matukio kutofanyika chaguzi za ndani, anaongoza chama ambacho watu wanazalishana tu ndani yake na anaongoza Chama kila mbunge wake anahaha pa kutokea ili 2020 apate pa kurejesha kiti na ulaji wake.
Nimefurahi kuwa leo zimepigwa gia mbili muhimu na zimetupa fundisho muhimu: gia moja ya mlimani na gia moja ya gerezani.
Tutafakari gia gani imekiki?
Na hapa ndipo Rais Magufuli labda kwa huzuni na kuwaonea huruma _Teamgeagerezani_anawaonea huruma akiwakumbusha "Mzee kawambie, wafuate sheria, waende kwa gia makini ya mlimani, la sivyo watajikuta wanapiga gia magerezani."
Ni mimi Mwamba (tamka mara 3) wa Kaskazini.