Ninaagiza jengo hilo kuwa libomolewe ndani ya siku 30 kwa gharama za mmiliki na akikaidi atalipishwa faini ya asilimia mbili ya gharama ya kuendeleza pasipokuwa na kibali kwa kila siku hadi atakapotekeleza agizo hilo, alisema Profesa Tibaijuka na kuongeza;
Makazi haya yanatakiwa kujengwa majengo yasiyozidi ghorofa 10, lakini katika hili ghorofa ambalo linatakiwa kubomolewa kwanza kiutaalamu halikuzingatia vigezo kutokana na kujengwa kwenye kiwanja chenye mita 150 ambacho ni kidogo.