Niambieni wapendwa. Mimi sielewi ni namna gani haya makampuni ya simu yanavyotukata pesa zetu. Ni mara nyingi nimekuwa najiunga na kifurushi cha sh.3,000/ ili niweze kutumia kwenye internet na airtel. Cha ajabu, ninapotaka kuanza kutumia internet, huwa niaambiwa salio langu halitoshi. Nikaweka tena kiasi hicho hicho, napo niliambiwa kuwa hakitoshi. Nikaweka mpaka mara ya saba, pia majibu yakawa ni yale yale. Nikapiga simu kwa kutumial line hiyo hiyo iliyokuwa kwenye moderm, simu haikupokelewa licha ya kuambiwa kuwa mimi ni mteja muhimu. Nilendelea kupiga mpaka mara tano, hali ilikuwa ni ile ile. Pesa yangu sijui imepotea? Kampuni hii ni Airtel - Hakatwi Mtu
Hilo Wana JF, ni moja. La pili ni hili. nilijiunga na kifurushi cha Supacheka. Salio langu katika simu yangu lilikuwa ni sh. 45,000/-. Nikajiunga na kifurushi cha sh. 15,000/-. Hii ilikuwa kwenye tarehe za kati ya 16 au 17 mwezi wa nane, 2013. Nikawa na mategemeo kuwa mpaka mwisho wa mwezi wa nane, ningebakiwa na salio katika simu na kwamba salio la kifurushi litakapokwisha, nitapata ujumbe wa muda wa kifurushi kuisha. Cha ajabu ni kwamba, tarehe 31/8/2013, nilipata ujumbe kuniarifu kuwa muda wangu wa kifurushi umekwisha. Nilipoangalia salio, nikakuta hata akiba yangu yote haikuwepo tena.
Wana JF, naomba kueleweshwa, hivi niliibiwa au ndo mtindo wa sasa?