Gharama Za Simu Ndio Zimepanda Kiasi Hiki!?

Gharama Za Simu Ndio Zimepanda Kiasi Hiki!?

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,795
Reaction score
9,153
Jana Jumapili mida ya saa kumi na mbili jioni nimeongea kwa sekunde 10 tu nimetumia Shs. 40.56, yaani karibia Shs. 4 kwa sekunde. Hivi mitandao yote ni Hivyo hivyo au ninaotumia mimi tu?
 
Jana Jumapili mida ya saa kumi na mbili jioni nimeongea kwa sekunde 10 tu nimetumia Shs. 40.56, yaani karibia Shs. 4 kwa sekunde. Hivi mitandao yote ni Hivyo hivyo au ninaotumia mimi tu?

kweli mkuu,gharama naona zimepanda kuanzia ktk vifurushi mpaka kupga kawaida!BIG UP kwa serekali sikivu na makini ya jk.
 
mimi pia naona gharama zimepanda, ata nikipiga voda kwenda voda.
 
serikali isipokuwa makini na hili swala, tunawezaa tukajikuta tunatamani tena p.o box, gharama zote za kupiga, vifurushi viko juu.
 
Na bado,,.....tutakamuliwa sana waTz mpaka tutakapoamua kua na msimamo na sio akili za kushikizwa
 
Da kudadeki serikali inabana kwenye vitu muhimu tuuuu
 
nitawahoji,wanaoafiki hoja hii waseme ndio "ndioooooo"
ccm utaipenda
 
imepanda mkuu jaribu kuangalia kifurushi cha internet cha ttcl ambacho nilikuwa nakinunua kwa laki mbili kwa mwezi leo ni 229,000/-
 
Sabab ni kodi ya line za simu..makampuni inabidi yatafute namna ya kulipa kodi ya line kwa ajili ya wateja wao....Hii ndio serikali sikivu ya CCM
 
gharama zimepanda sana tena sana mfano halisi chungulia MPESA walivoamua kuua, kudadeki kutuma laki 4 unakatwa 1200 kutoa unapigwa elfu 4 na ushee jumla ya transaction hiyo ni zaidi ya elf 5500.
 
hivi hakuna uwezekano wa ku-review upya hizi kodi?
 
gharama zimepanda sana tena sana mfano halisi chungulia MPESA walivoamua kuua, kudadeki kutuma laki 4 unakatwa 1200 kutoa unapigwa elfu 4 na ushee jumla ya transaction hiyo ni zaidi ya elf 5500.

umeona enheee na tigopesa kutoa 500K ni 6000 kutoka 5000
 
Na bado tutawakamua kwenye kila kitu mkija kushtua ss tushakuwa mabilionea na pesa zetu hatuwek hapa nchin!Mlipoambiwa maisha bora kwa kila mtanzania labda hamkuelewa lakin labda sasa mmeanza kunielewa.Nitafaham hili itakapofika 2015,Arusha wangekuwa ni nchi now wangekuwa mbali sn kwan jamaa wameamua kumaanisha kuwa wamechoshwa na haya maisha
 
Kwenye kuvaa kofia, fulana na vitenge vya njano tunafurahia, sasa huo ni wakati wake wa kuvuna waathirika ni wote waliovaa ofa hizo na wale wasiovaa.
 
We are conned left, right and center. Poor hopeless tanzanian

True. Mi nimeamua kuachana za zile line nyingine nikabakiza moja tu. Hatua ya pili nimeachana na mambo ya nyimbo za miito ya simu. Hatua nyingine zitafuata baada ya kufanya tathmini ya hizi za awali.
 
Jana Jumapili mida ya saa kumi na mbili jioni nimeongea kwa sekunde 10 tu nimetumia Shs. 40.56, yaani karibia Shs. 4 kwa sekunde. Hivi mitandao yote ni Hivyo hivyo au ninaotumia mimi tu?

Mkuu hujajua kuwa serikali sikivu imeamua kuzifanya simu kuwa kama nyumba ndogo kwa watumiaji?, hadi tujute kwa nn tunatumia simu
 
tuache kulalamika sana, tukutane na wabunge wetu 2015 majimboni watakuja tu hasa hawa wa chama tawala coz wanautumia wingi wao bungeni kutuumiza walala hoi,jamaa wametusaliti na sisi tuwakatae.
 
Back
Top Bottom