Gharama za kukosa amani.

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,410
31,395
Wasomali wanaorudi kutoka Saudi hatarini


090602180512_somali-refugee386x217.jpg
Wakaazi wakiuhama mji wa Mogadishu

Picha hii na maelezo yamepatikana kutoka BBC swahili.com

Wakuu, nimeileta picha hii hapa jamvini kuwakumbusha baadhi yetu ambao kwa kutoelewa au kwa makusudi kauli zao na maandishi yao hayazingatii gharama za Amani. Ninafahamu kuwa zipo picha nyingi kama hizi zinazotia huzuni ambazo mumeshaziona.

Huyu Mwnamama amebeba mzigo wa mkeka ambao huenda una nguo,mashuka n.k. Pia amebeba godoro ambalo uzito wake kila mtu anaujua. Mkono mmoja amebeba taa kwasababu hajui huko aendako kiza ni kinene kiasi gani. Hajui mafuata ya taa atapata wapi la muhimu ni kuwa na taa kwanza. Mkono wa kulia amebeba kikopo sijui ni cha chakula au nini. Lakini kibaya zaidi amebeba kiumbe[mtoto] ambaye masikini ameletwa duniani bila kujua na sasa analipa gharama kwa asichokitenda wala kukijua. Nyuma yupo dogo ambaye amechoka na hajui wapi anaelekea akifuatiwa na mzee.

Fikiria kuwa upo mahali fulani duniani hapa na kisha unamuona huyo mwanamama ambaye ni Dada yako wa kuzaliwa, au mama yako au rafiki yako anakwenda asikokujua, jiulize utajisikiaje.Mimi hapa natokwa na machozi nikiangalia hii picha tu.!
Somalia ni nchi yenye watu wanaoongea lugha karibu moja na dini moja. Lakini ulafi wa madaraka na ufisadi ndio umewfikisha hapo.
Jiulize unapotoa kauli za uchochezi za kidini au kikabila hiki ndicho unachotaka kukiona?

Tusimame kidete kwa pamoja kuwapinga na kuwakataa viongozi kama akina Aideed, tubishane na kupingana bila kupigana, hata kama tofauti zetu ni za kisiasa au kiitikadi, basi kuwe na mpaka, tukijua kuwa uhuru wa mtu unaishia pale wa mwingine unapoanzia.
Tujue kuwa hakuna aliyepewa nafasi ya kuchagua kabila kabla hajazaliwa na kwamba hilo kabila lako ni bora kama la mwenzako, na imani ni utashi wa kiroho, kile unachokiamini si lazima mwingine akiamini na kwamba imani iwe yako na si yetu ili amani iwe yetu.
 
Back
Top Bottom