Gharama za gesi na upatikanaji wake

Bw Harage

Member
Aug 31, 2007
15
16
wadugu bloggers
Ninatatizwa na gharama za umeme na Mkaa kwenye kupikia, naomba kama kuna anayejua gharama za mtungi mmoja wa gesi na wapi naweza kuipata hapa Dar. Mkaa sio bei sana lakini sio clean, umeme unapanda kwa hiyo budget yangu ambyo ni limited itanitesa kiasi. Kwa mwenye ufahamu please naomba nijulishe!
 
Gesi inapatikana oryx kwa gharama kati ya sh 10,000 na 15,000 kwa mtungi wa kilo 6,sasa inategemea na familia yako kama bachela tu unaweza kutumia hata mwezi,ila tatizo gesi nayo sometimes inakuwa adimu hivyo kutishia kupanda kwa bei yake.Si hivyo tu unahitaji mtungi,regulator na jiko kama unataka kuenjoy matumizi yake ila unaweza kupika moja kwa moja toka kwenye mtungi kwa kupachika kichuma fulani hivi juu ya mtungi.
 
mie natumia Gesi home. Nilinnua Oryx au..hapa karibu na Kamata Junction ya Msimbazi na Pugu Road/Nyerere Road...Nasikia sasa wamehama nafikiri nenda ktk vituo vya Mafuta pembeni.

Kg 15/16 wanauza 30,000 sasa zamani ilikuwa 25,000. Mtungi wana kukopesha 45,000/=,(kama unao no need kulipa hio nenda no mtungi wako wakujazie), Jiko nafikiri Bei yake inategemea na matumizi yako..inafika 35,000/= na kuendelea.regulator+pipe inaweza fika 20,000-25,000/=
Go ahead Gesi nzuri ila GHARAMA...Rafiki yangu alie Qatar ananiambia mtungi wa kg30-32 kama 20-30,000 ya TZ...price Bongo ni twice as much...Sijui Uzalishaji wa Songas umefikia wapi au tusubiri Gesi mpya ya MKURANGA...
 
yeah asante kwa kumchambulia vizuri,sema pipe inategemea anataka ya urefu gani lakini bei yake ilikuwa 2500 na regulator ilikuwa 15,000
 
Naomba kuuliza!!!
Ni ORYX peke yake wanaosambaza? na mimi nafikiria kuopt lakini makazi ninayoishi hakuna ORYX -(Mtwara)
 
Nawashukuru sana waheshimiwa, ni ajabu sana kuona kuwa tuna gesi lakini ni bei sana! Hapa ni kama serikali inatuhimiza tutumie Mkaa, yaani wanatuhimiza tuendelee kutoa support ya kuharibu misitu!
 
Back
Top Bottom