Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Serikali ya Tanzania na kampuni za ujenzi za Uturuki na Ureno zimesaini mkataba wa ujenzi wa Reli kutoka Dar mpaka Morogoro kwa gharama ya dola bilioni 1.21. Awamu ya kwanza ya reli hiyo kutoka Dar mpaka Morogoro itakuwa na urefu wa kilomita 300 kati yake kilomita 205 ni njia kuu na 95 ni njia za kupishania treni.
Ujenzi huo utahusisha pia uzio wa usalama kutokana na reli hiyo kutumia umeme pamoja na ujenzi wa vivuko kwa watu na wanyama. Mradi huu utagharimikiwa na serikali pamoja mkopo kutoka nje, Haya makampuni yote yalishinda na kupewa tenda ya ujenzi wa reli hii baada tenda kutangazwa kwa wazi.
Mwaka 2012 serikali ya Tanzania ilizindua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar mradi huo ulifadhiliwa na mkopo kutoka Benki ya Exim ya China kwa gharama ya dola 1.225, ujenzi huu pia ulisimamiwa na kampuni China Petroleum and Development na kampuni nyingine China Petroleum Pipeline Engineering Corporation. Ina maana mradi huu tenda haikutangazwa kimataifa.
Kitendo cha serikali ya awamu ya tano kuweka wazi tenda ya ujenzi wa reli ya Dar - Morogoro inafaa sana kupongezwa kwani suala la ujenzi wa bomba la mafuta limekuwa na maswali mengi sana haswa ukiangalia gharama ya ujenzi wa bomba hilo ni kubwa sana, haiwezekani kwa China kutoa mkopo halafu kuwa na makampuni ya kichina kupewa tenda ya ujenzi wa bomba hilo bila kutangazwa ili makampuni mengine kushiriki. Kuna uwezekano mkubwa kama hiyo tenda ingetangazwa kimataifa gharama ya ujenzi wa bomba hilo isingefika dola bilioni 1.225.
Napenda kumpongeza Waziri wa Ujenzi Proff. mbarawa kwa kusimamia na kuwa wazi katika hatua ya kwanza ya ujenzi wa reli ya kati kwa kazi hiyo Watanzania tumeanza kuona kazi ya serikali ya awamu ya tano kwa vitendo na uwazi.
Naomba nisahihishe kichwa cha thread ni bomba la Gesi sio mafuta.