Gharama halisi ya kusajili Kampuni huko BRELA ni kiasi gani?

vipik2

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
2,803
2,185
Ndugu wapendwa naomba msaada ili nipate kujua gharama halisi ya kusajili Kampuni huko BRELA mpaka nipate certificate zote itakuwa Kama Tsh ngapi?
 
Hakuna gharama maalumu mkuu ila tenga 50,000 ya name reserv alafu ukutane na kamlolongo chakupata gharama za usajili
 
Ndugu wapendwa naomba msaada ili nipate kujua gharama halisi ya kusajili Kampuni huko BRELA mpaka nipate certificate zote itakuwa Kama Tsh ngapi?
Dola 1000 sawa na milioni mbili unaletewa certificate popote ulipo.
 
Ndugu wapendwa naomba msaada ili nipate kujua gharama halisi ya kusajili Kampuni huko BRELA mpaka nipate certificate zote itakuwa Kama Tsh ngapi?
Gharama halisi za BRELA mpaka kupata Certificate
1. Gharama za BRELA kwa kampuni itakayokuwa na share capital kuanzia Tshs 20,000 mpaka Tshs 1,000,000 gharama yake utalipia BRELA Tshs 167,200
2. Lakini utahitajika uwe na Memorandum and Articles of Association na lazima isainiwe ma Mwanasheria kwaiyo kuna gharama ya kuandaliwa hii Memorandum na kusainiwa na Mwanasheria ambayo ni Tshs 100,000 hii itaambatana na Form 4B ambayo inapatikana kwenye mtandao wa BRELA nayo inahitajika kusainiwa na mwanasheria, pia kuna gharma za kutengenezewa sample ya muhuri ambayo ni Tshs 5,000 huu utawekwa kwenye form ya ethics and integrity. Na kama utaona tabu au mbali kufika BRELA nitakufanikishia kufanya usajili wa Kampuni yako.

Kama utahitaji namba zangu 0718887102
 
Mkuu Njoo nikusajilie kampuni kwa Tsh 250,000/= tu ndani ya dakika 15 fika ofisini Posta au piga 0712 450 136 au tuma sms
 
Mkuu Njoo nikusajilie kampuni kwa Tsh 250,000/= tu ndani ya dakika 15 fika ofisini Posta au piga 0712 450 136 au tuma sms
Ameuliza gharama mpaka kupata Certificate na hakusema anataka kusajili Kampuni, na unaposema njoo nikusajilie kwa Tshs 250,000 ikiwa mtu hajua gharama zingine utakuwa unakosea hizo Tshs 250,000 ni za kwako ukija kumwambia gharama za BRELA alipie tena atakuelewa kwaiyo unapaswa umfahamishe gharama za pande zote mbili
 
Back
Top Bottom