Ghana, Kenya na Malawi kufanyiwa majaribio ya chanjo ya kwanza ya Malaria duniani kuanzia 2018

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Chanjo ya kwanza ya malaria duniani itafanyiwa majaribio katika nchi za Ghana, Kenya na Malawi kuanzia 2018. Chanjo hiyo inafundisha mfumo wa kinga ya mwili kushambulia vijidudu vya malaria vinavyosambazwa na mbu.

WHO imesema chanjo hiyo inatarajiwa kuokoa maelfu ya maisha. Lakini bado haiko wazi kama itaweza kusaidia katika sehemu masikini zaidi duniani.

Chanjo hiyo inatolewa mara nne; mara moja kila mwezi kwa miezi mitatu na dozi ya nne miezi 18 baadaye.

Chanjo hii imeweza kuonesha mafanikio katika majaribio lakini haijajulikana kama itatoa matokeo hayo hayo katika "dunia halisi" ambapo upatikanaji wa huduma za afya ni hafifu. Hii ndio sababu inayopelekea WHO kufanya majaribio (pilots) katika nchi hizo 3 ili kuona kama programu kamili ya chanjo ya malaria inaweza kuanzishwa. Itaendelea kuangalia usalama na ufanisi wa chanjo hiyo.

Mpango huo wa majaribio utahusisha zaidi ya watoto 750,000 wenye umri kati ya miezi 5 na 17. Nusu ya watoto hao watapewa chanjo hiyo ili kulinganisha matokeo.

Ghana, Kenya na Malawi zilichaguliwa kwani zina programu kubwa za kupambana na malaria ikijumuisha kutumia vyandarua vya kuzuia mbu lakini bado zina idadi kubwa ya maambukizi.

Licha ya maendeleo makubwa, bado kuna 'cases' milioni 212 mpya za Malaria kila mwaka na vifo 429000.

Imetafsiriwa kutoka Malaria: Kenya, Ghana and Malawi get first vaccine - BBC News
 
Niwaza tu kama dawa ya UKIMWI itakuwa sokoni 2018 kama wanavyosema, chanjo ya malaria hali kadhalika itabidi tulime sana maana binadamu watakuwa wengi sana na vifo vitapungua.
 
Back
Top Bottom