GGM kuchelewesha fidia kwamkwaza Peneza

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Upendo Furaha Peneza, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) ameitaka serikali kutoa maelezo ni lini itawalipa fidia wananchi wa Geita ambao walipisha mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), anaandika Dany Tinason.

Amesema wapo wananchi ambao walipisha mgodi huo lakini hawajalipwa fidia zao hadi sasa jambo ambalo linaonekana kufumbiwa macho na serikali.

Awali katika swali la msingi la Deogratias Ngalawa, Mbunge wa Ludewa (CCM) alitaka kujua wananchi waliochangia ardhi ya yao kupitisha miradi watalipwa fidia lini.

Pia alitaka kujua miradi ya mkaa wa mawe wa Mchuchuma na Liganga kwamba, itaanza lini?

Akijibu swali hilo Dk.Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati na Madini amesema, wale wote ambao wanapisha maeneo yao kwa ajili ya kupisha shughuli za maendeleo, hufanyiwa tathimini na kisha hulipwa fidia.

Akizungumzia wale ambao wanatakiwa kuondoka katika maeneo ya migodi amesema, migodi huwajibika moja kwa moja kuwalipa fidia na pale muhusika asiporidhika huweza kufuata taratibu za kisheria.

Akizungumzia miradi ya Mkaa wa Mawe wa Mchuchuma na Chuma cha Liganga amesema, inasimaniwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Amesema miradi hiyo inaendelezwa kwa pamoja kati ya NDC lenye asilimia 20 ya hisa na Kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Company Limited ya China yenye hisa asilimia 80 kupitia kampuni ya ubia ya Tanzania.
 
Serikali inapaswa kuwasaidia walipwe fidia zao mapema ili waendelee na maisha yao sehemu nyingine, make kuwacheleweshea ni kuwafanya wakose imani na serikali yao.
 
Upendo Furaha Peneza, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) ameitaka serikali kutoa maelezo ni lini itawalipa fidia wananchi wa Geita ambao walipisha mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), anaandika Dany Tinason.

Amesema wapo wananchi ambao walipisha mgodi huo lakini hawajalipwa fidia zao hadi sasa jambo ambalo linaonekana kufumbiwa macho na serikali.

Awali katika swali la msingi la Deogratias Ngalawa, Mbunge wa Ludewa (CCM) alitaka kujua wananchi waliochangia ardhi ya yao kupitisha miradi watalipwa fidia lini.

Pia alitaka kujua miradi ya mkaa wa mawe wa Mchuchuma na Liganga kwamba, itaanza lini?

Akijibu swali hilo Dk.Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati na Madini amesema, wale wote ambao wanapisha maeneo yao kwa ajili ya kupisha shughuli za maendeleo, hufanyiwa tathimini na kisha hulipwa fidia.

Akizungumzia wale ambao wanatakiwa kuondoka katika maeneo ya migodi amesema, migodi huwajibika moja kwa moja kuwalipa fidia na pale muhusika asiporidhika huweza kufuata taratibu za kisheria.

Akizungumzia miradi ya Mkaa wa Mawe wa Mchuchuma na Chuma cha Liganga amesema, inasimaniwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).

Amesema miradi hiyo inaendelezwa kwa pamoja kati ya NDC lenye asilimia 20 ya hisa na Kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Company Limited ya China yenye hisa asilimia 80 kupitia kampuni ya ubia ya Tanzania.
Nyie Chadema, hebu acheni ujinga wenu, pelekeni majina ya wabunge wenu 19 wa viti maalum, pimeni pros na cons za kususa muone nini kina faida zaidi, hata kama sio kwa Chadema as chama, then waachieni fursa za ajira wanawake wenu 19, tena nashauri priority iwe ni kwa wale waliogombea majimboni.

Just imagine, mtu kama huyu kukosekana Bungeni?.
Acheni hizo, pelekeni majina.

P
 
Majimbo yote Tanzania ni viti maalum. Kuongezea tena viti maalum 19 ni kuongezea serikali hasara. Bakini Kama mlivyo na nguo za kijani. MAENDELEO hayana chama
 
Back
Top Bottom