Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,266
- 2,870
Geti na Ukuta wa Chuma
Ni asubuh nyingine kama kawaida Lusajo anaamka na kujinyoosha tayari kuanza kujiandaa kuelekea kazini, anakumbuka kuwa jana alisahau kununua mkate. Amejenga mazoea ya asubuh kupata kifungua kinywa kabisa kabla ya kwenda kazini. Anaamka na kukaa kwenye kitanda kwanza akiwa amevaa boxer. Anajinyoosha …halafu ananyoosha mkono kubonyeza kifungo ukutani kuwasha taa. Mara unapokuja mwanga anafinya macho yake kiasi na kuyafikicha. Anageuka huku na kule kana kwamba anaangalia au anatafuta kitu kisha anaamka na kujinyoosha tena.
Anaelekea bafuni kwa ajili ya kupiga mswaki na kuoga. Lusajo amemaliza chuo miaka miwili iliyopita akiwa amesomea Information Technology na ameajiriwa na Kampuni inayohusika na mambo ya IT akiwa kama IT Technician. Amepanga nyumba yenye vyumba viwili kimoja master bedroom,sebule ya wastani na jiko. Mara kadhaa hupenda kupika hasa inapokuwa weekend.
Katika nyumba hiyo wapo pia wapangaji wengine wawili nao wakiwa na nyumba kama yake . ni apartments. Sehemu tulivu kila mtu akiwa busy na mambo yake. Leo anapooamka anakumbuka jana hakununua mkate. Na huwa hawezi kuondoka bila kutia kitu tumboni. Anapiga mswaki na kuoga halafu anavaa kaptula na tshirt nyepesi anatoka nje ya geti kwenda jirani kwa Dada Asha ambaye hutengeneza Chapati nzuri sana. Asha ni mwenyeji wa Tanga. Amepanga nyumban kwa mzee Rashid. Ana kama mwaka mmoja sasa toka ahamie hapo akiwa anaishi na mdogo wake wa kike.
Inasemekana Asha aliolewa na Baadaye akaamua kuachana na mumewe. Na hivyo akaondoka kwa mumewe huko Mwenge na kuja kuishi Ubungo. Ni dada anayejipenda mcheshi na mwenye kujiamini. Rangi ya ngozi yake ni maji ya kunde. Mwenye mwili kiasi flan na kiuno kidogo. Alikuwa na umbo la kupendeza. Si mnene wa kutisha lakini pia si mwembamba . Alikuwa anaonekana kuwa na mapaja manene na malaini kutokana na kuwa akitembea kunaonekana mitikisiko flan. Ingawa mara nyingi alikuwa akivaa gauni refu au akijifunga khanga.
Mtaani alikuwa anafahamika sana kwa kutengeneza Chapat ,Sambusa,Vitumbua na Maandazi. Alikuwa akiamka asubuh sana saa tisa au kumi alfajiri na kuanza kutengeneza vitu hivyo na baadaye kuvipeleka kwenye Hotel mbalimbali. Kiuhalisia alikuwa ni mpishi mzuri sana na kwa wengine waliotaka vitu hivyo walikuwa walifika kwake kununua.
Lusajo anagonga na Asha anaitika “karibu” anasukuma mlango na moja kwa moja anafika kwenye kibaraza cha uani kwa asha. Asha amekaa amejitandaza akikaanga chapati. Lusajo anamtizama jinsi ambavyo ameutandaza mwili wake akiwa amekaa kwenye kiti kifupi na miguu ameitanua . amejifunga khanga na kichwan amevaa kofia ya kuficha nywele zake. Na blauzi ya mikono mifupi pembeni yake kuna majiko mawili na vyombo kaadha vyenye chapati, vitumbua na sambusa.
“Karibu uncle” anamkaribisha huku akiendelea na kugeuza chapati upande mwingine. Lusajo anakaribia na kumwambia anahitaji chapati sita. Asha anahesabu chapati Sita anazifunga kwenye foil vizuri na kumwekea mfukoni mteja wake na kisha anamkabidhi. Lusajo anazipokea na kutoa pesa.
“mamaaah we kaka unanitafuta ubaya mtoto wa watua subuh hii…jamani mi ntapata wapi change ya 10,000?” anasema huku akitabasamu na kuamka. Anapoamka… Lusajo anamtizama na bahati mbaya khanga inapanda juu na kuacha wazi sehemu za mapaja na ndani kuonekana. Asha amevaa nguo ya ndani nyeupe. Haraka anajifunika na kwa aibu anaondoka akiharakisha kueelekea ndani hili ni kosa jingine kwa upande wake, maana napotembea haraka mwili wake unatikisika. Baada ya dakika moja anasikika kutoka ndani akisema “ uncle change hamna kama hutojali naomba uje kuchukua baadaye. Au nikupe uende nayo ukipata utaniletea”
Lusajo anamjibu “ hamna shida sister kaa nayo ntakuja baadaye” akiwa anaondoka akili ya Lusajo inawaza alichoona kwa asha. Asha kwa nje alikuwa maji ya kunde. Lakini ndani ya miguu yake alionekana kuwa na weupe flan mzuri kama wa embe dodo lililoivia mtini. Alionekana kuwa soft na ….. aliwaza hilo kwa haraka sana akakumbuka ile chupi nyeupe ambayo kiukweli ilikuwa ni rangi nzuri kwa wadada. Alikumbuka namna ilivyokuwa imevimba pale mbele.alishtuka tu akiwa amefika getini na kuwa anapaswa atoe funguo afungue kuingia ndani. Akaenda ndani akachemsha maji haraka kwa jiko la gesi na kuchukua maziwa ya kopo,kahawa,sukari na chapati zake tatu akaziweka kwenye sahani aanze kupata kifungua kinywa.
Alipokamata chapati ile laini mawazo yake ghafla yalihamia kwa Asha na kile alichoona asubuh. Mwili wake ulisisimka akawaza ulaini wa chapati zile na utamu ule akaufananisha na mpishi. Kiuhalisia alikuwa kama ametekwa na mawazo yale. Alitikisa kichwa ili akili ikae sawa ….akamaliza kunywa chai na kwenda kujiandaa aondoke kwenda kazini. Njia nzima alikuwa akiwaza tukio lile la asubuh. Kilichomshangaza ni kwa nini tukio lile limekaa kichwan mwake kwa muda mrefu na wakati halikuwa jambo kubwa sana. Alikuwa kila anapotizama anamwona asha akinyanyuka. Kila akifumba macho anamwona asha akinyanyuka kusimama.
Kazini aliendelea na kazi zake kama kawaida tofaut ya leo na siku nyingine ni kuwa leo alikuwa kimya sana. Watu wengi walimfahama Lusajo kwa story na ucheshi mwingi. Lakini huyu wa leo alikuwa mkimya sana na mwenye kuonekana amezama kwenye dimbwi la mawazo. Alikuwa akiomba siku iishe haraka arud nyumban akapumzike. Ni mara kadhaa amekuwa akimwazia Asha lakini ilikuwa kikawaida tu kuwa huyu dada ni mzuri lakini hakuweza dhani kama yule dada angekaa kichwan kwa siku ile namna ile.
Jioni ilikuwa inakaribia lakini kwa mwendo wa pole pole sana. Ilikuwa ni siku isiyo na haraka..siku iliyopoa kabisa machoni na moyoni mwa Lusajo. Kila mara alikuwa akingalia saa na wakati mwingine alikuwa kama haiamini saa yake na kujikuta akiuliza kwa wenzie. Alikuwa akiwaza namna ambavyo ataenda kuonana na Asha. Kuchukua change. Alikuwa akiona aibu pia kwa kiasi flan na anaamini pia asha alikuwa ameona aibu na ndo maana hakutoka nje na kuamua kumwambia akiwa ndani kuwa hamna change. Lakini zaidi alikuwa amepatwa na mfadhaiko. Ni muda mrefu sasa Lusajo hakuwa na mpenzi. Alikuwa ameamua kuishi maisha yake peke yake baada ya kutengena na mpenzi na aliyekuwa amemchagua kama mchumba Anneth.
Toka kipindi hicho hakuwa na hamu tena ya kupenda. Aliteseka kwa miezi mingi pasipo kula vizuri akifikiria yale waliyotenda pamoja na siku moja tu kama umeme uwakavyo na kuzima Anneth akasema kuwa anadhani hawezi endelea kuwa pamoja naye.ilikuwa kirahisi sana. Anneth alisahau miaka zaidi ya miwili waliyokuwa pamoja toka akiwa Chuo. Baadaye alipokuja kusikia anneth ana mahusiano na mfanyabiashara mmoja mkubwa. Aliumia sana. Aliumia kwa kuwa aliachwa katika kipindi ambacho alihitaji sana kuwa an mtu wa karibu. Lusajo alikuwa ametoka kumpoteza baba yake na mdogo wake ambao walifariki kwenye ajali ya gari. Yeye akiwa kaka shughuli zote za msiba na kila kitu kilimwangukia yeye. Dada yake alikuwa akisoma mwaka wa kwanza chuo.
Alikuwa amechoka kimaisha.pesa zake zote alizitumia kwenye msiba na pia kumuuguza mama yake ambaye alilazwa kwa miezi miwili kutokana na mshtuko. Hapo Lusajo alifikia hatua ya kuuza gari lake aweze kumhudumia mama yake. Alihitaji mapenzi na faraja. Kama ni kidonda Anneth alikuja kumwagia pilipili. Ilikuwa maumivu ndani ya maumivu. Kwa moyo ulionyong’onyea, kwa shingo upande na maumivu yasiyosemekana moyoni Lusajo alimruhusu Anneth aende. Alitumia week nzima kumbembeleza pasipo mafanikio. Ikafikia hata Anneth akawa hapokei simu wala kujibu msg.
Hapo Lusajo akaukumbatia moyo wake, akajikunyata kwenye kona ukutani akilia na kulia akimlilia Anneth arudi. Maskini anneth hakusikia kilio hicho, hakuona machozi ya Lusajo. Siku hiyo Lusajo analia hivyo chumban Anneth alikuwa Ufukweni kwenye Hotel moja ya kisasa amevaa bikini na kujizungushia taulo huku akinywa Mvinyo wa bei ghali sana. Pembeni yake alikuwepo Phill Kashia au walio karibu naye walipenda kumwita Cash Man. Cash Man alikuwa ni mfanyabiashara mwenye maduka ya Nguo, Kampuni ya kuuza magari toka Japan na pia miradi kadhaa ambayo ilimfanya awe ni mmoja ya watu ambao pesa ndogo ndogo haziwasumbui. Alifahamika sana maana mwenye pesa hakosi marafiki.
Sasa Lusajo akili yake imejileta tena kwenye mapenzi safari hii na dada wa mtaani..hakuelewa kama ni mapenzi au ni tamaa. Lakini siku zote aliamini mambo ni kama pande mbili za shilingi moja. Unampenda mtu na pia unataman kuwa naye kimapenzi. Alisema ambaye huwez mtamani ni mama au dada yako tu. Lakini kwa wengine watu baki ikiwa ana mvuto utamtamani.
Jioni ilipofika Lusajo aliagana na wenzie na haraka kuanza kuelekea kituo cha magari yaendayo kasi kurudi kwake Ubungo. Alitembea kwa haraka kidogo kuelekea kituoni. Akiwa njiani alikuwa akiwaza kuwa akifika tu nyumban atabadili nguo na kuelekea kwa asha kuchukua change yake. Aliwaza atamwongelesha nini zaidi asha?
Alifika Ubungo mwisho kituoni na kushuka . haraka sana akaanza kuelekea kwake. Aliona kama bado angechelewa hivyo akaita bajaji na kumwelekeza dereva anakoenda. Alifika kwake akavua nguo na kwenda oga. Muda nao ulikuwa umesogea na jua limesha zama tayari kukaribisha giza kuchukua nafasi yake. Alichagua tena kaptula na tshirt nyepesi sabab ya joto. Akajipulizia marashi na kuvaa saa. Akajitizama kwenye kioo na kuona alikuwa sawa. Akatoka chumban tayari kwenda kwa sha kuchukua change. Aliwaza na kuona ni bora tu avae sandals. Lusajo alivaa sandals na kuanza kutembea kwenda kwa asha……
ITANDELEA