neggrer
Senior Member
- Oct 26, 2016
- 180
- 83
Habari za mida wakuu!
Ni matumaini yang mko vema kiafya.
katika harakati za kutafuta maisha kwny jamii zetu tulio wengi tumewah kupitia, tunapitia na wengne tunatarajia kupitia maisha ya geto.
kwa tafsiri yangu binafsi geto ni nini?
geto ni chumba (single) kinachotumiwa na mtu kwa matumizi mbalimbali (multipurpose), kubwa likiwa ni kwaajili ya malazi. wengine geto huliita store kwa maana kwamba geto utakuta kimetunzwa kila kitu kinachohtajika ili mtu aweze kuishi.
Kwa "asilimia kubwa" geto hutumiwa na vijana katika umri wa kati kwa wastani wa miaka 20-30, ambacho kwa wengi ni kipindi cha mpito kuelekea utu uzima.
Katika kipindi hiki vijana wenye umri husika hulazimika kukaa geto kwa sababu mbalimbali. Mfano wa makundi ya wahusika ni wanafunzi wa vyuo, waajiliwa wachanga, na wachakalikaji wengine.
Kwa tafsiri ya haraka, geto ni chumba ambacho kimsingi kinapaswa kumilikiwa na mtu mmoja kwa matumizi binafsi au wakae wapenzi (ME na KE) au wanandoa (Mke na Mume).
Kutokana na sababu flani flani, inatokea geto moja wanakaa marafiki wa kinsia moja (washkaji au mashost), hii kwa baadhi ya wapangishaji huikataa na wengine hutoza kodi kwa kila mmoja (individually).
Je, wewe ni miongoni mwa wahusika tajwa kwenye kichwa cha uzi huu?
Tunaweza kushare experience katika haya.
-Una uzoefu gani na maisha ya geto?
-Changamoto gani umewahi kukumbana nazo katika maisha ya geto?
-Visa na vimbwanga, maudhi na vituko?
- kitu unacho kimiss ni kipi? ( kwa waliotoka)
-Ni kipi utakimiss? (ukitoka)
- Tabia za wenye nyumba?
-Uliwezaje kutoboa mpaka kumiliki mjengo wako?
-Maisha ya geto yamekufunza nini mpaka sasa?
Kwa wanasheria mnaweza kutupa hints za kisheria kuhusu masuala yahusuyo geto mf. masuala ya notis n.k
Ahsanteni
Sent using Jamii Forums mobile app