GESI YETU/YAO (Dondosha hapa)

GESI YETU/YAO (Dondosha hapa)

Ranks

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Posts
2,583
Reaction score
1,098
Baba wa Taifa hayati Mwalimu NYERERE aliendesha Nchi/Taifa kwa kilimo,viwanda na utalii kiasi,rasilimali zetu zote zilitunzwa kwa kiasi kikubwa.

Mapema kabisa twende pamoja suala hili la gas sio suala la wao Wana Mtwara dhidi ya wana Dar es salaam na na sehemu nyinginezo kama Mwanza nk bali ni suala la yao watawala au ni ya kwetu sote wana wa nchi na Afrika kwa ujumla kwanza.

Tuna maana gani kuimba wimbo wa Taifa kuiombea Afrika ibarikiwe ilhal tumebarikiwa na hatukithamini kile tulichobarikiwa kuwa nacho mkononi,Ardhini.??? Bahati nzuri au mbaya baba yangu mwenye utu Rais mstaafu Ally H. Mwinyi akapokea kijiti cha Taifa.,Utu ukamponza,wachawi wa kijani wakachomeka dhambi zao pale Zanzibar"wakalizika AZIMIO LA ARUSHA"kimtindo kwa hila.

Bahati nzuri kwao akaingia Che Nkapa,hamna kucheka,kweli uchumi ukajaribu kusimama kisaniisanii kwani tungetaka kupaiza uchumi wetu huu ulikuwa ndio wakati.Ukweli ni kwamba tulipata wehu wa kutokujithamini na kudharauliana.

Tulianza/walianza kutupatupa mali zetu ovyo kwa mikataba ya kipumbavu na kiuendawazimu kama majuha tena kwa kasi kubwa ya ajabu. Sipendi kutumia neno awamu lakini hapa tulipo awamu hii tumeendeleza kutapanya mali zetu/zao ovyo,tuliambiwa kwa kasi zaidi na ari zaidi kwa min ajili ya maisha bora kwa kila mtanzania/wao watanzania.

Kama una kumbukumbu au ushahidi wa lolote ktk mchakato kuanzia kutambulika hadi kupatikana kwa gesi hii makubaliano au mikataba DONDOSHA HAPA kwani pia sio ajabu kwa hali halisi tunavyoishi na kuendesha nchi yetu ukapatikana ulaghai,usaniisanii ama uvundo wa kukirihisha ndani ya mradi huu husika.

Tusidanganyane kwamba mapungufu makubwa yaliyojitokeza na kutuacha uchi kwenye mikataba ya huko nyuma hayatajitokeza(hayatajirudia) tena kwa kutoa matamko bila ya kusimamia sheria na misingi bora ya TAIFA ENDELEVU.

Ni wendawazimu tu wanaoweza kuvumilia mikataba mingi mibovu naya kijuha tuliyoingia/waliyoingia kama TAIFA. HEBU TUSEME INATOSHA,mali hizo tulizokwisha zitoa tangu tufungue milango na madirisha hadi mwisho bado hatujaona faida yake (matunda) kwa wananchi.

TUSUBIRI KWANZA TUPATE KATIBA MPYA YENYE MTIZAMO HASI KWA TAIFA NA WATU WAKE. Kama hayati Mwalimu aliweza kuendesha nchi bila ya kugusa hizi raslimali,SIE UHARAKA NA ULAZIMA NI WA NINI?NA ULAZIMA HUO KWA SASA UNATOKA WAPI? Je ni haki ya uhuru rasilimali nyeti,adimu na aghali kumnufaisha MTANZANIA ktk kipindi adhimu kwa ujira kama kibarua(MANAMBA) kama viongozi wetu wanavyohubiri???KUMBUKA HII NI MALI YETU SOTE,hivyo basi akili ya _ _ _ _ _ changanya na zako.
 
Back
Top Bottom