Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 876
Katika kutafuta ufumbuzi wa suala la gesi kusafirishwa toka Mtwara kuja Kinyerezi Dar, je tujiulize kwanza,mpango huo umeanza lini?
Naomba kwa mwenye kumbukumbu atuambie kwenye ilani ya CCM 2010 waliahidi nini kwa wana Mtwara mwaka huo?
Je mgombea wao katika kusaka kura tu bila kuangalia maneno gani anatumia kuwaambia wana Mtwara aliwaahidi nini?
Haya nayasema kutokana na matukio yaliyowahi kutokea huko nyuma kutokana na ahadi za Kikwete kutoa kila mahala alipoenda ili mradi yeye kuwadanganya tu huku akijua hana uwezo wa kutekeleza.
Je si kweli kuwa ilani yao na ahadi ya Kikwete inasema gesi ya Mtwara itabakia huko na wata process huko wengine watapelekewa baadae? KUNA AHADI NYINGI ALIZITOA PAPO KWA PAPO BILA KUANGALIA MADHARA YAKE.
Kwa wepesi wa Kikwete kuahidi, je si kweli kuwa aliwaahidi wana Mtwara gesi itabakia huko Mtwara ili kuendeleza mji huo na wana Mtwara kwa ujumla?
Tujikumbushe ya mahakama ya Kadhi.Ilani iliwaahidi lakini kufika kwenye utekelezaji mgogoro.
Wana Ruvuma tuliahidiwa umeme wa gridi ya Taifa lakini hadi leo hata nguzo kusimikwa tu kwa kudanganyishia hakuna.
Tazama juu ya ugunduzi wa makaa ya mawe Ruvuma.Alisema kupatikana kwa makaa hayo kutaondoa kabisa tatizo la umeme Ruvuma.Lakini leo hii makaa hayo ya mawe yanasafirishwa kwenye malori na kupelekwa Dar.
Kikwete hana uwezo wa kusimamia ahadi zake.Kama anabisha waje wasaidizi wake waseme kama Ruvuma hawakuahidi kuunganisha kwenye gridi ya Taifa?
Haya ndio mambo yanayomgharimu Kikwete.Na kama kila alipoahidi wananchi wangekuwa na kumbukumbu kama ya wana Mtwara kufuatilia basi leo hii kila mahala kungekuwa hakukaliki ni fujo mtindo mmoja.Lakini nafuu wanayoipata ccm ni kuwa wananchi wengi ni mbumbumbu hawajui kuhoji wala hawakumbuki waliahidiwa nini.Sisi wengine tukisema vijiweni ahadi zao wanatuambia uwongo hatukuahidi hayo na ahadi zote tumetekeleza.
ADUI MKUBWA WA CCM KWA SASA NI WANANCHI KUJUA HAKI ZAO NA SI WAPINZANI
Gharama ya uwongo malipo yake ni ghali sana.