Gesi Mtwara: Kikwete apingwa

Gesi Mtwara: Kikwete apingwa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,342
Gesi Mtwara: Kikwete apingwa

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

Posted Jumapili,Januari6 2013 saa 13:25 PM
Kwa ufupi
VYAMA VYASEMA KWA NAMNA YOYOTE ILE GESI HAIONDOKI MTWARA, VYATAKA PROFESA MUHONGO AONDOLEWE, CCM MTWARA KUKUTANA

SAKATA la wananchi na baadhi ya wanasiasa kupinga usafirishwaji wa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, limechukua sura mpya, baada ya vyama vya siasa nchini kuungana na kutumia jukwaa kumpinga Rais Jakaya Kikwete, vikisisitiza kuwa gesi haitaondoka Mtwara.
Vyama hivyo pia, vimemtaka Rais Kikwete kumwondoa katika wadhifa wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa madai kuwa ametoa kauli ya kuwakejeli wananchi wa mkoa huo.

Vyama hivyo vinapinga gesi asilia itayotarajiwa kuanza kuvunwa katika Mkoa wa Mtwara, kusafirishwa kwa bomba kwenda jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa haitawanufaisha.

Hata hivyo, Rais Kikwete katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, alisema siyo sahihi kwa wakazi wa Mtwara kuizuia gesi isisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa sababu rasilimali hiyo ni ya Watanzania wote.

Wakihutubia kwa nyakati tofauti mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Soko Kuu, mjini Mtwara jana jioni, viongozi wa vyama hivyo walisema kwamba hawako tayari kuona rasilimali za nchi zikiendelea kusababisha umaskini kwa wananchi, badala ya kuwakomboa."Ukicheka na nyani utavuna mabua, wenzetu kwenye madini walicheka nao na wamevuna mabua, sisi hatuko tayari…; Tunatambua kuwa mamlaka ya nchi yapo mikononi mwetu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama Kikwete amesema kwa namna yeyote ile gesi itatoka, basi sisi tunamwambia, kwa namna yeyote ile gesi hatoki," alisema Mohamedi Salim mjumbe wa umoja huo kutoka NCCR- Mageuzi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Mohamedi Sinani amethibitisha kufanyika kwa kikao hicho kesho Jumatatu.
Aliongeza: "Kwanza, tunataka Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo aondolewe katika wadhifa huo kwa sababu analeta propaganda za kisiasa kwenye masuala nyeti yanayohusu maisha ya watu."
Kwa pande wake, Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Mustafa Nchia alisema kuwa wataandamana hadi Serikali itakaposikia kilio chao na kwamba kwa kuanzia wanataka Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, aondolewe mkoani humo akidai aliwatusi wananchi kwa kuwaita wapuuzi.


Akizungumza na Mwananchi Jumapili alisema: "Tutakutana Jumatatu kwenye kikao cha Kamati ya Siasa Mkoa, baada ya hapo nitawaambia nini msimamo wa chama mkoa kuhusu gesi."
Wadadisi wa mambo wanasema kuwa kikao hicho pia kitajadili na kutoa tamko juu ya msimamo wa mbunge Murji na ule wa chama hicho Wilaya ya Mtwara Mjini kupinga mradi huo.

Katika mkutano huo, makamu mwenyekiti wa umoja huo, Uledi Abdallah alimpongeza Kamanda wa Polisi mkoani humo, Maria Nzuki, kwa kuruhusu maandamano hayo na kuwataka wananchi kuondoa woga katika kusimamia rasilimali zao, mradi wasivunje sheria.
Mikutano hiyo itaendelea kesho katika Viwanja vya Bima na keshokutwa katika Viwanja vya Nkanaledi.


Awali, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo unaojumuisha vyama vya siasa, Uledi Abdallah aliliambia gazeti hili kuwa, kwa siku tatu mfululizo wanatarajia kuendesha mikutano mikubwa ya hadhara katika Viwanja vya Soko Kuu, Bima na Mkanaledi.

Uledi ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Wilaya ya Mtwara Mjini alisema: "Januari 13, tutawapokea viongozi wa NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia, wabunge wote wanne wa chama hiki."

Kamati ya Siasa ya CCM mkoa kukutana
Wakati mkutano huo wa vyama vya siasa ukifanyika, Kamati Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara, inatarajiwa kukutana kesho ili kujadili mgogoro wa gesi na kutoa msimamo wao.


Kamati hiyo itakutana huku tayari kukiwa na mgongano baina yao, kutokana na chama hicho Wilaya ya Mtwara Mjini, sambamba na mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji kuunga mkono wananchi wa mkoa huo kupinga kusafirishwa kwa gesi hiyo inayovunwa katika Kijiji cha Msimbati mkoani humo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara Mjini, Ali Chinkawene, hivi karibuni alisema kuwa msimamo wa chama chake ni kuungana na wananchi, kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam na kwamba Serikali inapaswa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme mkoani Mtwara, badala ya Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa msimamo huo siyo wake binafsi, bali ni maazimio ya vikao halali vya chama hicho vinavyowakilisha wanachama na kwamba, historia ya mikoa ya kusini jinsi ilivyonyimwa maendeleo ilitumika na wajumbe kujenga hoja yao hiyo.

Kwa uamuzi huo, CCM Mtwara Mjini, inaungana na vyama tisa vya awali vilivyokuwa vinapinga gesi kupelekwa Dar es Salaam, ambavyo ni Chama cha Wananchi (CUF), Chadema, NCCR-Mageuzi, SAU, TLP, APPT Maendeleo, ADC, VDP na DP, vikiwa na kaulimbiu ya "Gesi kwanza vyama baadaye, hapa hakitoki kitu."

Umoja wa vyama hivyo tisa, ndiyo uliratibu maandamano ya Desemba, 27 mwaka uliopita kupinga mradi huo wa gesi.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji, ameweka wazi msimamo wake wa kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam na kuongeza kuwa yupo tayari kuvuliwa ubunge, kama ikibidi kufanya hivyo katika kutetea masilahi ya wananchi.

Tofauti na Murji, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia ambaye ni Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Mbunge wa Newala, George Mkuchika Waziri wa Ofisi ya Rais, Utawala Bora wao wanaonyesha kuunga mkono mradi huo.

Kwa nyakati tofauti mawaziri hao wamekaririwa wakiwatia moyo wananchi kuwa mradi huo unalenga kuwanufaisha wao na Taifa kwa jumla, licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wananchi.

Novemba, 20 mwaka jana wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, Ghasia alizomewa na wananchi pale alipojaribu kutetea mradi huo.

Licha ya Ghasia na Mkuchika kuwa siyo wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, wabashiri wanasema kuwa kuna uwezekano wa kikao hicho kuwa kigumu kutokana na baadhi ya wajumbe wake kuonyesha wazi kutounga mkono hoja ya gesi kupelekwa Dar es Salaam.

"Keshokutwa (kesho) kutakuwa na kazi ngumu. Wapo wajumbe waliopania kutetea masilahi ya wananchi…wanaona chama kitakufa iwapo wataunga mkono gesi kuondoka, watu wanajipanga kwa hoja siyo ushabiki," kilisema chanzo
chetu ambacho ni kada wa CCM.

CUF kuandamana Dar
Jumuiya ya Vijana wa CUF imesema kuwa itafanya maandamano makubwa jijini Dar es Salaam, kuunga mkono wananchi wa Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Katani Katani alisema kuwa maandamano hayo yatafanyika siku yoyote kuanzia leo kwa lengo la kuonyesha kwamba hata vijana wa CUF na chama chao kwa jumla kinapingana na mpango wa Serikali kuhusu mradi huo.

Mbunge apinga
Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu amesema kuwa haungi mkono maandamano kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwenda jijini Dar es Salaam.

Alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, ambapo pamoja na mambo mengine, alisema kuna haja kwa Serikali na wananchi kukaa pamoja na kujadiliana jambo hilo kwa kina, badala ya kulipinga kwa kutumia maandamano.

Abdallah Bakari, Mtwara na Aidan Mhando, Fidelis Butahe, Dar.


 
jk na serikali yake dhaifu wamelikoroga...
Kauli yenu tumeisikia!
Ni dhahiri wana Mtwara wameamka kutoka kwenye usingizi wa pono uliokuwa umewafunga miaka mingi.
Tunaendelea kuwaunga mkono, na kuwaomba msikubali kudanganywa kama ilivyokuwa zamani kwa kapelo, Tshirt na vitenge 2015!
Mwalimu alisema 'Inawezekana, timiza wajibu wako'

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!
 
Narudia kusema hili swala la Gesi Mtwara ni mtego na njia ya kumfukuza Prof....Nia ni kuwa wizara hii ishikiriwe na wasanii na kuonesha kuwa na elimu kubwa sio kigezo cha uongozi..hivyo tuendelee kuongozwa na wajanja wanjanja siku za mbele.
 
Tuko pamoja, Mtwara ni Gesi kwanza then Magamba out. Uroho na Ubinafsi wa JK umeshatusaidia kuing'oa CCM Mtwara HATUGEUKI NYUMA TENA mpaka lengo letu litimie.
 
Wana Mtwara Kazeni buti ni haki yenu wenzenu wote sijui Kiwira,mererani Mwadui,Kahama,Geita ,Nyamongo na kuingine kwingi kote huko hawajawahi kunufaika na chochote zaidi wanadhalirishwa
 
Hakuna mtego wowote, Muhongo kakurupuka kutoa kauli ambazo hakutakiwa azitoe sasa imekula kwake. Ukiwa na wadhifa wowote ule Serikali na inapotokea kwamba una msimamo tofauti na wananchi basi ni lazima uwe makini sana katika kuchagua kauli zako badala ya kuongea pumba kwa kuwaita wenyeji wa Mtwara wahaini, bila shaka kauli hizo pumba Muhongo sasa hivi anazijutia. Kishapoteza credibility yake kama Waziri wa Nishati na Madini ila wasiwasi wangu DHAIFU ataendelea kumkumbatia labda mpaka mwisho wa awamu yake.

Narudia kusema hili swala la Gesi Mtwara ni mtego na njia ya kumfukuza Prof....Nia ni kuwa wizara hii ishikiriwe na wasanii na kuonesha kuwa na elimu kubwa sio kigezo cha uongozi..hivyo tuendelee kuongozwa na wajanja wanjanja siku za mbele.
 
Mbatia anafuta nini huko wakati alishatukana watu juzi? Au anataka apigwe bakora alafu alete lawama?
 
Pengine I miss something...maana haya ma contract makubwa Africa, yanakuwaga yana ubabaishaji mkubwa sana nyuma yake. Hata hivyo, Why so much noises with gas....kama korosho zimewashinda watu wa Ntwara, gas watafanya nayo nini bila watu wengine kuingilia kati?
 
Hakuna mtego wowote, Muhongo kakurupuka kutoa kauli ambazo hakutakiwa azitoe sasa imekula kwake. Ukiwa na wadhifa wowote ule Serikali na inapotokea kwamba una msimamo tofauti na wananchi basi ni lazima uwe makini sana katika kuchagua kauli zako badala ya kuongea pumba kwa kuwaita wenyeji wa Mtwara wahaini, bila shaka kauli hizo pumba Muhingo sasa hivi anazijutia. Kishapoteza credibility yake kama Waziri wa Nishati na Madini ila wasiwasi wangu DHAIFU ataendelea kumkumbatia labda mpaka mwisho wa awamu yake.

Ahhh haya ndg..utakuja kuniambia siku si nyingi subiri...,huyu hafai pale wewe aliwekwa kupitisha mwanaharamu apite...na ameepuka baadhi ya mitego lazima awekewe zenge amablo inabidi asimamie serikali na ndilo analotolea maamuzi mkuu hivyo ndio litakalomuondoa subir...
 
Pengine I miss something...maana haya ma contract makubwa Africa, yanakuwaga yana ubabaishaji mkubwa sana nyuma yake. Hata hivyo, Why so much noises with gas....kama korosho zimewashinda watu wa Ntwara, gas watafanya nayo nini bila watu wengine kuingilia kati?
Kama huna hoja kaa kimya au uliza ujuzwe kwanza ndio ujenge hoja. Hebu tueleze ni kwa namna gani korosho imewashinda wanainchi wa Mtwara, tuanzie hapo kwanza ili upate darasa kabla hatujaendelea na hoja ya gesi.
 
Pengine I miss something...maana haya ma contract makubwa Africa, yanakuwaga yana ubabaishaji mkubwa sana nyuma yake. Hata hivyo, Why so much noises with gas....kama korosho zimewashinda watu wa Ntwara, gas watafanya nayo nini bila watu wengine kuingilia kati?

Unatutindinganye wako! limbulunga chani!
 
Kumbuka kauli kauli za Muhongo mara tu baada ya kuteuliwa "mgawo wa umeme sasa Tanzania utakuwa historia" "makampuni yote ya nje ya uchimbaji madini ambayo yapo nchini kwa miaka mitano na kuendelea lazima yaanze kulipa 30% kodi mara moja au yafungashe virago vyake" kumbe ni usanii mtupu!!!!


Ahhh haya ndg..utakuja kuniambia siku si nyingi subiri...,huyu hafai pale wewe aliwekwa kupitisha mwanaharamu apite...na ameepuka baadhi ya mitego lazima awekewe zenge amablo inabidi asimamie serikali na ndilo analotolea maamuzi mkuu hivyo ndio litakalomuondoa subir...
 
Ghana wamesimamisha uchimbaji wa mafuta mpaka wajifunze makosa ya mikataba na wizi wake unavyo athiri umma kutoka Nigeria. Hapo serikali imefanya makosa ya kutowasaidia wananchi hella za logistic support walipoanza kuchimba gas. Logistic support ni pesa za mchimbaji za kuwapooza wananci ambapo hujenga barabara, kuweka shule zote mapaa mapya na madeski darasanai, kujenga maabala ya hospitali na kuweka hapo katika kijiji ka mji ka kisasa.

sasa utakuta hapa nchini, pesa hizo za kusaidia wananchi huliwa na waziri ambaye huweka mikataba na kuwafanya wananchi waziki kuletewa kero na mchimbaji.

kama serikali ingewapa logisstic support wananchi wa Mtwara, mambo haya wananchi wangeona haya kuandamana. sasa na nyie wamanda mbinga mashariki, mbamba bay na wanyakyusa wa Kyela, mafuta yanategemewa kuchimbwa ziwa nyassa. Je mtakubali mchimbaji aje achimbe bila hata kuwapa logiztic support?

mambo haya ndiyo serikali ya ghana imejifunza jinsi ya kuwabana mawaziri waroho kuto wadhurumu wananchi wa maeneo yachimbwayo mafuta raha na faida ya kuwa na rasilimali maeneo yao.
hongera sana wakadhi wa mtwara mmewafungua macho watu wote wa vijiji vyenye madini na mafuta kudai haki zao.
 
Kumbuka kauli kauli za Muhongo mara tu baada ya kuteuliwa "mgawo wa umeme sasa Tanzania utakuwa historia" "makampuni yote ya nje ya uchimbaji madini ambayo yapo nchini kwa miaka mitano na kuendelea lazima yaanze kulipa 30% kodi mara moja au yafungashe virago vyake" kumbe ni usanii mtupu!!!!

Sawa hayo nayajua ila kumbuka huyo ni serikali hivyo hayo ni matamshi ya serikali sio yake binafsi. Ndio maana nakuambia fikiri zaidi ya hapo utajua anatumika kwa muda.
 
Profesa Muhongo ni kati ya Watanzania wakweli wa nafsi na matendo. Alitamka anachoamini, kuwa kudai rasilimali asilia iliyopo kwenye eneo fulani la Tanzania ni lazima iwanufaishe wakazi wa eneo hilo pekee kwanza, na wengine baadaye ni uhaini. Kwa kuwa Watanzania wamezoea kauli za kisanii, kauli za kuzungukazunguka, ni dhahiri wataichukia kauli ya prof. Tunafahamu uwezo wa Prof. Muhongo kitaifa na kimataifa, kama Watanzania wataendekeza ukambatiaji wa kauli za kubembeleza, kauli za kisanii hata kama zinauzunguka ukweli, prof. anaweza kuondoka lakini atakayekuwa amekula hasara siyo prof. bali ni Watanzania wenye tamaa ya kuongozwa na wanafiki wasio na uwezo na kuwakataa watanzania wenye uwezo, dhamira na umahiri wa kiutendaji.
Hakuna mtego wowote, Muhongo kakurupuka kutoa kauli ambazo hakutakiwa azitoe sasa imekula kwake. Ukiwa na wadhifa wowote ule Serikali na inapotokea kwamba una msimamo tofauti na wananchi basi ni lazima uwe makini sana katika kuchagua kauli zako badala ya kuongea pumba kwa kuwaita wenyeji wa Mtwara wahaini, bila shaka kauli hizo pumba Muhongo sasa hivi anazijutia. Kishapoteza credibility yake kama Waziri wa Nishati na Madini ila wasiwasi wangu DHAIFU ataendelea kumkumbatia labda mpaka mwisho wa awamu yake.
 
Unazungumza kwa hisia au una takwimu. Hebu nitajie makampuni ya madini ambayo bado hayajaanza kulipa corporate tax ya 30%.
Kumbuka kauli kauli za Muhongo mara tu baada ya kuteuliwa "mgawo wa umeme sasa Tanzania utakuwa historia" "makampuni yote ya nje ya uchimbaji madini ambayo yapo nchini kwa miaka mitano na kuendelea lazima yaanze kulipa 30% kodi mara moja au yafungashe virago vyake" kumbe ni usanii mtupu!!!!
 
Serikali gani unayozungumzia? Hii Serikali DHAIFU inayotoa kauli zilizojaa usanii kila kukicha!?

QUOTE=JF-MBUNGE;5394609]Sawa hayo nayajua ila kumbuka huyo ni serikali hivyo hayo ni matamshi ya serikali sio yake binafsi. Ndio maana nakuambia fikiri zaidi ya hapo utajua anatumika kwa muda.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom