Gerson Msigwa anajishushia heshima mitandaoni

Gerson Msigwa anajishushia heshima mitandaoni

NIPOSINGO

Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
11
Reaction score
39
Tangu akiwa Msemaji wa Serikali, amekuwa cheap sana huyu jamaa.

Hivi sasa wizara aliyoko haina afisa habari au waziri? Naona ana-dominate yeye tu mitandaoni

Kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu alipaswa awe mtendaji/mtaalamu/mwanataaluma zaidi wa wizara yake sio kutafuta cheap popularity kila uchwao.

Sasa ona mfano hapa anajibizana na Babalevo. Kweli hadhi ya Ukatibu Mkuu anaijua huyu? Chawa kama Babalevo anamkejeli KM atakavyo, huku Msigwa yeye akihisi ndio socialization

Statements nyingine anazotoa zilipaswa kutolewa na waziri mwenyewe lakini Msigwa yupo mstari wa mbele

Katibu Mkuu gani anajipost mara anakimbia na mijasho, mara anacheza mziki, mara analima shambani na bibi, yaani ni full comedy

Ni maoni yangu ashauriwe kubadilika mara moja.

IMG_7570.jpg
 
poleni tz hamña raic hapoo juu ndo tatizo lilipoanzia.
Umepiga kwenye mshono mkuu🙏🙏
Siyo karibu mkuu tu, wengi wamepewa vyeo kwa vimemo, ndomana wanapwaya, hawafit nafas walizopewa, mfano makamishna wasaidizi wa Ardhi, wengi wao ni vilaza Hakuna,kisa vyeo vya vimemo, ila uwezo mdogo, tutafika lakini👌
 
HV katibu mkuu kulima ,kukimbia na kucheza nayo iwe shida ,mnataka umuone wapi kulima kwako Ni tatizo

Hatters acheni hzo muacheni afurahie maisha yake
 
Shida ni nini hasa.life style yake ama utendaji wake??Kama ni kuhusu utendaji wake kiofisi, sina comment, lkn kama ni kuhusu life style yake..wewe pia inabidi uache ushamba, hivyo ni vyeo tu, haviondoi personality ya mtu...Anawapa somo, watu kuwa simple...nchi zilizocivilized ubabe wa kujimwambafai kisa kiongozi uliishapitwa na wakati...
Acha jamaa aishi anavyotaka, amposti mama yake etc..ndo furaha yake..na hayo ni mambo yake binafsi hayatuhusu sisi...
 
Nakazia hapa
 
Back
Top Bottom