Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,454
- 32,980
GEREZANI DAY 2025
Gerezani ina umuhimu wa pekee katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Katika jambo ambalo sikulitegemea wala kutarajia ni siku Salum Matimbwa aliponirushia ukurasa mmoja wa shajara (diary) ya baba yake, Abdallah Matimbwa aliyokuwa akiandika wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mzee Matimbwa akiishi Mtaa wa Kupata na Msimbazi.
Abdallah Matembo ameandika habari za Mwalimu Julius.
Haya nimeeleza leo katika Gerezani Day.
Mtaa wa Kipata na Sikukuu ndipo ilipokuwa nyumba ya Clement Mohamed Mtamila.
Barua ya Julius Nyerere aliyeandikiwa wa waajiri wake Wamishionari ikimtaka achague moja, kazi ya ualimu au uongozi wa TANU ilijadiliwa nyumbani kwa Clement Mtamila na Kamati Kuu ya TANU wajumbe wakiwa Bibi Titi Mohamed, Tatu bint Mzee wote hawa wakazi wa Gerezani.
Kikao cha watu watatu kupokea taarifa ya kusajili TANU kilifanyika nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata na New Street na kikao hiki kilikuwa cha watu watatu: Abdulwahid Sykes, Ally Sykes na Julius Nyerere na Mama Mwenye Nyumba Bi. Zainab (Mama Muni) alikuwapo.
Taarifa aliyofikisha Nyerere ni kuwa Msajili amekataa kuisajili TANU sababu Nyerere hakuwa na orodha ya wanachama wa TANU.
Hii ndiyo moja ya mengi yaliyopitika Gerezani wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika.
Mzee Mtamila alikuwa Mwenyekiti wa TANU Nyerere akiwa Rais wa TANU.