Genymotion, emulator bora ya android kwenye PC

@ msaada kwenye kuiweka genymotion kama simu hizo link naona hazina kitu
 
download nox ndio emulator nzuri kwa sasa
Chief hii pc unaionaje na kwa hiyo bei maana nataka pc ya kufanya simple editing kwa ajili ya documentary zangu fupi fupi
HP PAVILLION 24 ALL IN ONE PC
PRICE: 1,599,000/= + VAT
SPECIFICATION:
INTEL:I5-7200U/CI52.50GLV PROCESSOR
8GB/1-DIMM RAM
1TB/7200RPM HARD DRIVE
DVDRW MR GBE
802.11B/G/N+BT
WEBCAM INTEL-HD620/IGP
23.8IPSFHD
W/ SPEAKERS W10H-64
 
ni ghali mkuu kwa pc isio na battery.

waweza nunua laptop ya hizo specs kwa around 1m,

ila kama umeipenda hivyo ilivyo itafanya editing ndogo ndogo kwa software zinazokubali quicksync kama cyberlink powerdirector na vegas pro.
 
Pc gani nzur ya all in one naweza kupata kwa milion moja chief
asili ya all in one siku zote zinauzwa bei ghali. na kwa maisha yetu huku ya umeme kukatika mara kwa mara kwa mimi naona kama hazimake sense sana. ila unaweza ukanunua kama unazipenda.

hio ya 1m niliokuambia ni laptop. zenye 6th/7th generation kama hio all in one ulioitaja.

unaweza ku assemble all in one yako mwenyewe kwa kutumia monitor na mini pc ambayo unaibandika nyuma ya monitor ila ni ngumu kupata hivi vifaa hapa Tz.

na hata hizo all in one ni ngumu kuzipata Hapa tz, naweza kukuangalizia yenye unafuu online ila kuipata hapa itakuwa ni ngumu.
 
Nitatafuta laptop mkuu asante sana kwa ushauri
kama shida ni kioo kikubwa utakuja kununua monitor baadae. ni rahisi tu ku connect laptop na monitor. tena utapata monitor nzuri yenye kioo kizuri kushinda hizo display za all in one za bei rahisi.
 
kama shida ni kioo kikubwa utakuja kununua monitor baadae. ni rahisi tu ku connect laptop na monitor. tena utapata monitor nzuri yenye kioo kizuri kushinda hizo display za all in one za bei rahisi.
Hivi sina weza kupata NUC nzuri nikai connect na tv ya LG Inches 24 via hdmi nikatumia wireless keyboard na mouse?
 
Hivi sina weza kupata NUC nzuri nikai connect na tv ya LG Inches 24 via hdmi nikatumia wireless keyboard na mouse?
thats exactly nilipomaanisha unaweza uka assemble all in one yako. unanunua mini pc kama nuc kisha unaipachika nyuma ya monitor na keyboard na mouse.

ila usinunue tv ya inch 24 itakuwa na resolution ya HD tu utaharibu macho yako, tafuta monitor zinakuwa na resolution kubwa. kibongo bongo monitor ni rahisi kuliko tv. used kkoo around laki 2 sometime chini ya hapo.

monitor ya inch 24 inakuwa na full HD au Quad HD.
 
kama shida ni kioo kikubwa utakuja kununua monitor baadae. ni rahisi tu ku connect laptop na monitor. tena utapata monitor nzuri yenye kioo kizuri kushinda hizo display za all in one za bei rahisi.
Hebu nieleweshe unaposema inakuwa ni HD nitaharibu macho, kwani monitor nzuri inafaa iwe vipi.
Mimi nilidhani tv ukigeuza monitor wakati wafanya editing ni nzuri zaidi
 
Hebu nieleweshe unaposema inakuwa ni HD nitaharibu macho, kwani monitor nzuri inafaa iwe vipi.
Mimi nilidhani tv ukigeuza monitor wakati wafanya editing ni nzuri zaidi
tv na monitor ni tofauti. tv mara nyingi inakaa mbali unakuta mita 2 mpaka 3 toka yalipo macho yako hivyo hata ikiwa na resolution ndogo haina madhara sana kwenye macho sababu ipo mbali.

ila monitor ni case nyengine yenyewe inakaa karibu na macho, hivyo utahitaji resolution kubwa zaidi.

unaweza fanya tv kama monitor ila iwe vile vile mbali kama unavyotumia siku zote na usiiweke juu ya meza ukakaa nayo karibu.

pia tv ina disadvantage nyengine kama vile
-refresh rate ndogo (sio tv zote)
-input lag
-connector chache etc

sema hizo disadvantage zinawahusu sana wanaocheza games na ma pro. kwa kazi za kawaida unaweza usione utofauti.
 
Mimi natumia laptop Packard Bell ina ram 4. i3 cpu 2.40ghz na simu yangu ni not2 ila sioni play store naomba msaada mkuu
Mkuu hizi laptop bado zinapatikana kweli, Vifaa vyake maana betri yangu imekufa imeshaanza kuniletea notification ya ku replace battery sijui napata wapi aisee...
 
Sitaziacha hizi emulator
NOX,MEmu na KOplayer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…