Genk yashinda 1-0 ugenini, Samatta aingia dk. 73

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
22,525
23,378
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, ameanza vyema na timu yake baada ya kusaidia ushindi wa bao 1-0 katika ligi ya Ubelgiji (Jupiter Pro League) dhidi ya wenyeji Mouscron Peruwelz. Bao la Genk liliwekwa kimiani na mshambuliaji wao Thomas Buffel

Samatta ameaminiwa na kocha wa timu yake, Peter Maes kwa kupangwa katika kikosi cha timu hiyo huku akiingia katika dakika ya 73 kuchukua nafasi ya winga wa kushoto Nikos Karelis

Ushindi huo umeipandisha timu yake kwa nafasi moja zaidi, na sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi yenye timu 16 kwa kujikusanyia pointi 38 baada ya kucheza mechi 25 nyuma ya vinara wa ligi Gent yenye pointi 52 baada ya kucheza mechi 24

Kila la heri Samatta, umeweka historia ya mtanzania kucheza Ulaya katika ligi ya daraja la juu.
 
Hakika tunamtakia kila la heri na awe balozi mzuri kwa wachezaji chipukizi na wenye nia ya kufuata nyendo zake. Waamini tu penye nia pana njia. Juhudi, nidhamu, maarifa, nia, ndoto, kutokukata tamaa, nk. humletea mtu mafanikio aliyo yatarajia.
 
Hapo Bado mi sijaelewa samata aliingia uwanjani pindi timu ikiwa imeshashinda tayari ama ilikuwa bado haijashinda...???
 
Back
Top Bottom