Genius Kabisa (Akasome chuo kikuu)

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
51,622
Reaction score
74,001
Mtoto (dogo)-- Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne (4) kwani hili la tatu (3) halinifai

Mwalimu-- Kwanini unasema Hivyo ?

Mtoto(dogo)--- Nina Akili nyingi sana .

==BASI MWALIMU AKAMUELEZA MKUU WA SHULE NA MKUU WA SHULE AKAITISHA INTERVIEW KWA DOGO '==

Maswali ni Haya
==================
Mwalimu --- Kwenye ndege kuna matofali ishirini (20) tukitoa Moja (1) tukalidondosha chini yatabaki mangapi !?

Mtoto(Dogo)-- Yatabaki kumi na Tisa (19)

Mwalimu -- Nipe hatua za kumuweka Tembo kwenye fridge .

Mtoto(dogo)-- Unalifungua fridge una muweka Tembo kisha Unalifunga "..

Mwalimu -- Nipe hatua za Kumuweka Nyani kwenye fridge "-



Mtoto(dogo) -- Unafungua fridge unamtoa Tembo uliyemuweka .Una muweka Nyani kisha Unalifunga fridge ..

Mwalimu --Kuna sherehe ya siku ya Kuzaliwa kwa Simba Wanyama wote Wamekwenda " kasoro Mmoja .
(A)Ni nani ?
(B)Na kwanini ?

Mtoto(dogo)--
(A)Ni nyani
(B) Kwa sababu Tume muweka kwenye fridge

Mwalimu -- Bibi kizee Amevuka Mto Unaokuwaga na Mamba Wakali na Viboko Aliwezaje ?.

Mtoto(dogo)--Aliweza kwa sababu Mamba na Viboko wote Walikwenda Kwenye sherehe ya kuzaliwa Kwa Simba ..

Mwalimu -- Ingawa Bibi Kizee Alivuka Mto salama Lakini Baadae Alikufa Unadhani ni kwanini ? ..

Mtoto(dogo)-- Ni kwasababu Alidondokewa na Lile Tofali Tulilolitoa kwenye Ndege na kulitupa Nje ..

Mkuu Wa Shule Akajibu--- Huyu Dogo Akasome Chuo kikuu ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…