Kama pale kwenye uwanja mkubwa wa Arusha Secondary walivyopapiga! Mwanzo ilisemwa kuwa wachina wameomba kuweka kambi yao kwa muda wakati wakirekebisha barabara za mjini,baadaye wakabadili fence kutoka mabati kwenda tofali! Walivyoona kimya wakahamia na upande wa chini wa barabara,pale pana uwanja mkubwa unaoshuka hadi karibu na reli,wakazungusha mabati bila kufanya shughuli yoyote ndani,baadaye wakaanza kufyatulia matofali humo! Sasa hivi ni mali ya Beijing China construction limited! Upande wa juu ni yard ya magari,na chini ni sehemu ya material! Mchina ni adui mpya kwa mustakabali wa nchi!