Geita: Wafanyabiashara wafunga maduka wakishinikiza mwenzao mgeni kulipa kreti ya soda kama kiingilio

HIVI NI TANZANIA HII? MBONA KIZAMANI SANA NAUNGANA NA MFANYA BIASHARA HUYO ASILIPE ILI WAONDOKANE NA MAMBO YA KIZAMANI HUENDA MAMBO HAYO YANAENDANA NA USHIRIKINA ASIWAPE HIZO 12 ELF KAMA ANALIPIA MAMBO YOTE YA SERIKALI
 
Mambo ya vijijini ni ya ushirika sana hapo atalipa tu la hasha ajipange sana kukabiliana na swala la kutengwa kwenye kila kitu
Huyo jamaa atakuwa mkinga au mchaga, yaani anaonyesha ni bahiri, ana kiburi pia anajitambua kimtindo Ila mwisho wa siku itam-cost tu. Ukienda kwa waroma ishi kama waroma, ukeinda kwa washamba jifanye na wewe mshamba...kuwa kama kinyonga.
 
Yuko vizuri ndiyomaana kawakazia,hata mimi nisingelipa,watanilazimishaje kujiunga na umoja ambao mimi sitaki,akaze hivyohivyo,na ikiwezekana afungue duka aendelee kupiga pesa.Akiweka msimamo,ninao uhakika kua ataheshimika sana hapo kijijini.Namsihi akaze,huo ndiyo uanaume sasa.
Siyo kutengwa, unakuta katoto kamoja kamekata moto. Labda kama na yeye yupo vizuri kwenye hiyo sector
 
JAMAA WAMEKUTANA NA MSHIRIKINA MWENZAO,WAO WANATAKA WAMROGE TU BIASHARA ZAO ZIENDE KOMBO,KAWASTUKIA!
Serikali iwafutie leseni hao wafanyabiashara sababu za Kufunga maduka haziko kwenye masharti ya leseni.
Afisa biashara wahi kumaliza huo mgogoro kabla hujatbuliwa na Magufuli .Mkuu wa mkoa na wilaya zigo lenu hilo
 
Atahama mwenyewe huyo bila kufukuzwa.

Waandishi mrudi hapo kijijini baada ya mwezi.
 
Yan mimi mwenyewe leo nimenunua kiwanja nakuta mwenyekiti ananiambia inabid nitoe elf 12 kwa ajili ya kunikaribisha kwenye mtaaa.... Kazi kwel kweli af n mjin tu....

Najuta kwann nimeondoka kwenye kupanga

Ila siwez goma maana najua nguvu ya uma n kali
Wafanyabiashara kijiji cha Nyamigana kata ya Kagu wilayani Geita wamefunga maduka yao na kugoma kuendelea na biashara baada ya mfanyabiashara mgeni aliyehamia kijijini hapo kugoma kutoa kreti moja ya soda kama kiingilio.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Mugwe Sabuni amesema wafanyabiashara hao zaidi ya 20 wamefunga maduka yao kwa siku nne sasa wakishinikiza mfanyabiashara huyo, Frank Lucas kulipa Sh12, 000 ya kreti ya soda kama kiingilio kitakachomwezesha kuendelea na biashara.

Sabuni amesema amefanya jitihada kutatua mgogoro ili wananchi zaidi ya 300 wa kijiji hicho wapate huduma bila mafanikio baada ya pande zote mbili kuwa na msimamo usiobadilika.

Mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo Robart Chale amesema wana utaratibu wao wa kulipia kiingilio kinachojenga umoja.

"sisi tunataka alipe kama halipi aondoke kwenye eneo letu maana huu ni utaratibu wetu akileta kreti ya soda wote tunakunywa" amesema.

Amesema wapo wafanyabiashara 40 na kila mmoja lazima alipe kiingilio kwenye kikundi na ambae hayupo tayari kulipa aondoke kwenye kijiji hicho.

Mfanyabiashara anayetakiwa kulipa Sh12,000, Frank Lucas amesema hayupo tayari kulipa kiingilio hicho kwa kuwa hakipo kwenye utaratibu wa malipo ya Serikali.

“Nililipa Sh20,000 kama kiingilio cha kijiji na mtendaji alinipa taratibu zote, kwenye hizi taratibu hakuna kiingilio cha wafanyabiashara," amesema Frank.

Mkazi wa kijiji hicho, Eliakim Kasoga amesema mgomo huo umewaathiri wananchi kwa kuwa hadi maduka ya dawa za binadamu yamefungwa na hawawezi kununua kitu chochote, kulazimika kwenda katika vijiji jirani.
 
When in Rome dance like Romans, unaenda kucheza kwangaruu sijui nini nani atakuelewa?

Jamaa mwenyewe ana jina la mbabe mmoja Marekani Frank Lucas halafu anashindwa kutoa kreti sijui

NB Geita ina watu wapumbavu sana mnafunga maduka kisa kreti la soda wacha ccm itawale milele
 
Wafanyabiashara kijiji cha Nyamigana kata ya Kagu wilayani Geita wamefunga maduka yao na kugoma kuendelea na biashara baada ya mfanyabiashara mgeni aliyehamia kijijini hapo kugoma kutoa kreti moja ya soda kama kiingilio.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Mugwe Sabuni amesema wafanyabiashara hao zaidi ya 20 wamefunga maduka yao kwa siku nne sasa wakishinikiza mfanyabiashara huyo, Frank Lucas kulipa Sh12, 000 ya kreti ya soda kama kiingilio kitakachomwezesha kuendelea na biashara.

Sabuni amesema amefanya jitihada kutatua mgogoro ili wananchi zaidi ya 300 wa kijiji hicho wapate huduma bila mafanikio baada ya pande zote mbili kuwa na msimamo usiobadilika.

Mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo Robart Chale amesema wana utaratibu wao wa kulipia kiingilio kinachojenga umoja.

"sisi tunataka alipe kama halipi aondoke kwenye eneo letu maana huu ni utaratibu wetu akileta kreti ya soda wote tunakunywa" amesema.

Amesema wapo wafanyabiashara 40 na kila mmoja lazima alipe kiingilio kwenye kikundi na ambae hayupo tayari kulipa aondoke kwenye kijiji hicho.

Mfanyabiashara anayetakiwa kulipa Sh12,000, Frank Lucas amesema hayupo tayari kulipa kiingilio hicho kwa kuwa hakipo kwenye utaratibu wa malipo ya Serikali.

“Nililipa Sh20,000 kama kiingilio cha kijiji na mtendaji alinipa taratibu zote, kwenye hizi taratibu hakuna kiingilio cha wafanyabiashara," amesema Frank.

Mkazi wa kijiji hicho, Eliakim Kasoga amesema mgomo huo umewaathiri wananchi kwa kuwa hadi maduka ya dawa za binadamu yamefungwa na hawawezi kununua kitu chochote, kulazimika kwenda katika vijiji jirani.

Wasukuma tubadilike hii ni aibu
 
Yuko vizuri ndiyomaana kawakazia,hata mimi nisingelipa,watanilazimishaje kujiunga na umoja ambao mimi sitaki,akaze hivyohivyo,na ikiwezekana afungue duka aendelee kupiga pesa.Akiweka msimamo,ninao uhakika kua ataheshimika sana hapo kijijini.Namsihi akaze,huo ndiyo uanaume sasa.
Kuuza kipindi hiki siyo sawa, wanaweza wakamfuata live wakamfanyia kitu kibaya.
 
Nimekaa sana bushi tena geita hiyo hiyo hao hawabadiliki na hata mamlaka zao zinajua ni mpka ukubaliane nao ndio maana wamepiga siku nne si ndogo anyway ni yao

Back
Top Bottom